• HABARI MPYA

    Thursday, April 02, 2026

    SIMBA SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 UWANJA WA MEJA JENERALI ISAMUHYO


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Suleiman Mwalimu Abdallah dakika ya 25 na beki wa kati Muivory Coasta, Ismaël Olivier Touré dakika ya 45’+2.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 34 katika mchezo wa 15 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
    Kwa upande wao Coastal Union baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 15 za me hi 17 sasa nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 UWANJA WA MEJA JENERALI ISAMUHYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top