• HABARI MPYA

    Thursday, April 30, 2026

    MBEYA CITY NA MASHUJAA FC HAKUNA MBABE, SARE 1-1 SOKOINE


    TIMU ya Mbeya City imelazimishwa sare ya bila mabao na Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 14 ikizidiwa pointi nne sasa na Mashujaa iliyo katika nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 20.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY NA MASHUJAA FC HAKUNA MBABE, SARE 1-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top