• HABARI MPYA

    Friday, May 15, 2020

    VIGOGO TFF WATUHUMIWA ‘KUBUGIA’ FEDHA ZILIZOTOLEWA NA MHESHIMIWA RAIS DK MAGUFULI KUSAIDIA SOKA

    Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
    TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imesema kwamba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetumia vibaya baadhi ya fedha zikiwemo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana, Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
    Fedha hizo ni Sh. Bilioni 1 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON) zilizofanyika Dar es Salaam mwaka jana.
    Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia John Mbungo amesema leo Jijin Dar es Salaam kwamba TFF baadhi ya watuhumiwa kutoka TFF wamekwishaitwa na kuhojiwa, na nyaraka mbalimbali zimechukuliwa.
    Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) na Makamu wake, Wilfred Kidao (kushoto) wanakabiliwa na tuhuma nzito ya ubadhirifu wa fedha

    Brigedia John Mbungo amesema kwamba watu hao wana hiari ya kurejesha fedha ama kusubiri uchunguzi ukamilike.
    Kwa upande wao TFF wametolea ufafanuzi tuhuma hizo, wakidai kwamba haikupokea fedha hizo na wala haijui matumizi yake.
    “TFF kupitia kwa Katibu Mkuu wake (Wilfred Kidao) jana ilitoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo, na inarudia tena kuwa hazikuingia katika akaunti za TFF, na wala haihusiki kwenye matumizi yake,”imesema taarifa ya TFF leo na kuongeza;
    “Vilevile TFF inaendelea kusistiza kuwa hakuna fedha yoyote iliyopokea wakati wa fainali hizo zilizochezwa Uwanja wa Taifa pamoja na Uwanja wa Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Taarifa ya TFF imesema inaamini vyombo vyenye mamlaka vinafanyia kazi suala hilo ili kubaini fedha hizo ziliingia kwenye akaunti ipi na matumizi yake yalikuwaje.
    Kamati Kuu ya Maandalizi ya AFCON U17 2019 ilikuwa chini ya Mwenyekiti Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Makamu Mwenyekiti wa Leodegar Tenga ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Mtendaji Mkuu wa Kamati hiyo ni Henry Tandau.
    Kamati nyingine zilikuwa ni ya Miundombinu iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Paul Makonda, Makamu wake Yusuph Singo ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo na Wajumbe Sunday Kayuni, Leslie Liunda, Nassor Idrissa, Mohamed Kiganja na Mhandisi Davis Shemangale.
    Kamati ya Masoko na Habari; Kelvin Twissa (Mwenyekiti), Angetile Osiah (Makamu), Dk. Hassan Abbas, Dk. Omari Swaleh, Iman Kajula, Tido Mhando.
    Fedha na Mipango; Doto James (Mwenyekiti),, Mohamed Dewji (Makamu), Dk. Seif Muba, Bernard Lubogo, Paul Bilabaye, Jacquelline Woiso na Cornel Barnabas.
    Usafiri na Malazi; Mhandisi Ladislaus Matindi (Mwenyekiti), Abubakar Bakhresa (Mwenyekiti), Aziz Abood, Alhaj. Ahmed Mgoyi, Mheshimiwa Ahmed Shabiby, Dk. Maige Mwakasege Mwasimba na Shebe Machumani.
    Uratibu Utalii; Dkt. Khamis Kigwangala (Mwenyekiti), Allan Kijazi, Devotha Mdachi, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Hoyce Temu, Leah Kihumbi (Mkurugenzi Sanaa) na Athuman Jumanne Nyamlani.
    Itifaki; Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mwenyekiti), Mndolwa Yusuph, Filbert Bayi, Mkurugenzi Uwanja wa Ndege JNIA, Happiness Luangisa, Alex Makoye Nkenyenge na Alhaji Idd Mshangama.
    Tiba na Udhibiti wa Dawa za Kusisimua Misuli; Profesa Lawrence Museru (Mwenyekiti), Dk. Paul Marealle, Dk. Edmund Ndalama, Dk. Christina Luambano na Daktari Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Hiiti Sillo.
    Sheria na Taratibu; William Erio (Mwenyekiti), Dk. Damas Ndumbaro, Edwin Kidifu, Ally Mayai na Khalid Abeid
    Ulinzi na Usalama; IGP. Simon Siro (Mwenyekiti), Michael Wambura, CP. Andengenye – Zimamoto, CP. Lazaro Mambosasa – Polisi Kanda ya Dar-es-Salaam, Mkuu wa Askari wa Usalama Barabarani, TISS na Jonas Mahanga.
    Rasilimali Watu; Dk. Francis Michael (Mwenyekiti), Allan Kijazi, Wane Mkisi, Juliana Yassoda na Gerald Mwanilwa.
    Tanzania haikufanya vyema kwenye michuano hiyo baada ya kutolewa hatua ya makundi kufuatia kushika mkia katika kundi lake, A ikizidiwa kete na Nigeria na Angola zilizotinga Nusu Fainali na Uganda iliyomaliza nafasi ya tatu.
    Cameroon ndiyo waliotwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuwafunga waliokuwa wapinzani wao Kund B, Guinea kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa Aprili 28, mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIGOGO TFF WATUHUMIWA ‘KUBUGIA’ FEDHA ZILIZOTOLEWA NA MHESHIMIWA RAIS DK MAGUFULI KUSAIDIA SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top