• HABARI MPYA

    Wednesday, July 03, 2019

    RASMI IBRAHIM AJIBU MIGOMBA AMEREJEA SIMBA SC KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Ajibu Migomba amesaini mkataba wa miaka miwili kurejea klabu yake ya zamani, Simba SC kutoka kwa mahasimu, Yanga SC.
    Taarifa ya Simba SC leo mchana imesema kwamba Ajibu ameamua kufanya maamuzi sahihi ya kurudi nyumbani Msimbazi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
    “Safari ya mtoto kuishi mbali na nyumbani imefikia ukingoni. Ibrahim Ajibu ameamua kufanya maamuzi sahihi ya kurudi nyumbani Msimbazi, ndio amerudi na amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza na kuwapa furaha Wanasimba. Karibu nyumbani Ajibu,”imesema taarifa ya Simba.
    Ajibu anakuwa mchezaji mpya wa nane kusajiliwa Simba SC na wa tatu mzawa baada ya kipa Beno Kakolanya kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam na beki Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United ya Singida.
    Mtendaji Mkuu wa Simba SC Ibrahim Ajibu Migomba amesaini mkataba wa miaka miwili kurejea Simba SC
    Wengine watano ni wa kigeni, ambao ni Wabrazil mabeki beki Gerson Fraga Vieira ATK ya Ligi Kuu ya India na Tairone Santos da Silva kutoka klabu ya Atletico Cearense FC, mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva kutoka Bragantino, zote za Daraja la Nne nchini Brazil na viungo Msudan Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman na winga Deo Kanda kutoka TP Mazembe ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Pamoja na kusaini wachezaji wapya, SImba SC pia imewapa mikataba mipya wachezaji wake kadhaa wa msimu uliopita, wakiwemo kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala, Muivory Coast, Serge Wawa Pascal viungo Jonas Mkude, Mzambia Clatous Chama na washambuliaji Nahodha Mkuu, John Bocco na Meddie Kagere raia wa Rwanda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI IBRAHIM AJIBU MIGOMBA AMEREJEA SIMBA SC KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top