• HABARI MPYA

  Wednesday, July 03, 2019

  GHANA, CAMEROON, DRC NA AFRIKA KUSINI ZATINGA 16 BORA AFCON

  HATUA ya makundi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika imekamilisha jana kwa timu za Ghana, Cameroon, Mali, Tunisia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutinga hatua ya 16 Bora.  
  Mabao ya Jordan Ayew dakika ya 46 na Thomas Teye Partey dakika ya 72 yaliipa ushindi wa 2-0 Ghana dhidi ya Guinea-Bissau katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa New Suez huku mchezo mwingine wa kundi hilo ukimalizika kwa sare ya 0-0 baina ya Benin na Cameroon.
  Maana yake, Ghana na Cameroon zote imemaliza na pointi tano na wastani sawa wa mabao +2, hivyo kwa pamoja zinakwenda hatua inayofuata huku DRC na Afrika Kusini zikifuzu kama washindi wa tatu bora.

  Na bao pekee la Amadou Haidara dakika ya 37 lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 Mali dhidi ya Ismailia katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa Ismailia, huku mchezo mwingine wa kundi hilo baina ya Mauritania na Tunisia ukimalizika kwa sare ya 0-0.
  Kwa matokeo hayo Mali imeongoza Kundi F kwa pointi F kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Tunisia iliyovuna pointi tatu na zote zinasonga mbele.
  Cameroon, Ghana, Mali na Tunisia zinaungana na Morocco, Benin, Uganda, Senegal, Nigeria, Misri, Afrika Kusini, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Algeria, Guinea na Ivory Coast kwenda hatua ya 16 Bora itakayoanza Ijumaa.

  RATIBA HATUA YA 16 BORA AFCON

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GHANA, CAMEROON, DRC NA AFRIKA KUSINI ZATINGA 16 BORA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top