• HABARI MPYA

  Thursday, July 04, 2019

  AZAM FC YAMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MIWILI MSHAMBULIAJI ALIYEWIKA KAGERA SUGAR MSIMU ULIOPITA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC wamefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji, Abalkassim Suleiman Khamis aliyewika Kagera Sugar ya Bukoba msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Taarifa ya Azam FC leo imesema kwamba amesaini mkataba wa miaka miwili na anakuwa mchezaji wa nne mpya kusajiliwa na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, baada ya Idd Suleiman 'Nado' na Warundi Emmanuel Mvuyekure na Seleman Ndikumana.
  Nyota huyo alikuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita, wakati akiichezea Kagera Sugar, jambo ambalo limemfanya Kocha Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije, kumhitaji katika kikosi chake.
  Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' akimkabidhi jezi Abalkassim Suleiman Khamis baada ya kusaini

  Taarifa ya Azam FC leo imesema kwamba amesaini mkataba wa miaka miwili
  Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo nchini Rwanda, kikiwa kinajiandaa kutetea taji lake la Kombe la Kagame, iliyolitwaa mara mbili mfululizo, michuano inayotarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Julai 6-21 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MIWILI MSHAMBULIAJI ALIYEWIKA KAGERA SUGAR MSIMU ULIOPITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top