• HABARI MPYA

  Thursday, October 18, 2018

  MAYWEATHER AKUBALI KUPIGANA NA KHABIB, AMUONYA AWE NA NIDHAMU

  BONDIA Mmarekani, Floyd Mayweather amemuambia mbabe wa sanaa za mapigani wa UFC, Khabib Nurmagomedov  'njoo katika dunia yangu' akimkaribisha Mrusi huyo katika ulingo wa ngumi kwa pambano linalotarajiwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani Milioni 200.
  Mayweather amesema pato lake katika pambano hilo linaweza kuwa mara mbili alilopata wakati alipopigana na mbabe mwingine wa UFC, Conor McGregor mwaka 2017.
  Nurmagomedov alimpiga McGregor katika pambano la mchanganyiko wa sanaa za mapigano mjini Las Vegas mwishoni mwa wiki iliyopita kabla ya kusema anamtgaka Mayweather, ambaye amesema pambano hilo lazima lifanyike Jijini Nevada.

  Floyd Mayweather amekubali kupigana na Khabib Nurmagomedov katika pambano la wababe wa Conor McGregor

  "Oh, tutapigana. Ameniita. Hivyo, amekuja katika dunia yangu,", amesema Mayweather mwenye umri wa miaka 41.
  "Bosi wangu ni mimi mwenyewe. Hivyo, siwezi kusema nini kinachoendelea kwa mwisho wa Khabib. Lakini, kwa mwisho wangu, tunaweza kufanya liwepo (pambano).
  "Ninapomuangalia Khabib ninapata malipo tisa. Ni zaidi ya pambano la McGregor. Makadirio wastani wa zaidi ya dola Milioni 100 au zaidi nitapata. Nitasema kati ya dola Milioni 110 na 200 makisio,".
  Nurmagomedov alikuza rekodi yake ya mapambano ya kulipwa katika sanaa za mapigano mchanganyiko hadi mapambano 27 akishinda yote na kurejeshaa taji la UFC uzito wa Light baada ya kummaliza raundi ya nne McGregor katika pambao lililomalizika kwa utata.

  Floyd Mayweather alimpiga Conor McGregor mwaka jana katika masumbwi

  McGregor aliingia kwenye masumbwi kwa muda mwaka jana kwa kupigana na Mayweather, ambaye alifikisha mapambano 50 ya kupigana na kushinda yote akimsimamisha mbabe kutoka Ireland katika raundi ya 10.
  Bingwa wa zamani wa uzito wa tofauti, Mayweather hakuweza kumkalisha chini McGregor, kitu ambacho Nurmagomedov alikifanya Oktoba 6 ukumbi wa T-Mobile Arena kabla ya kumlazimisha mpinzani wake kujiuzulu.
  Akiomba pambano hilo, Nurmagomedov amemuambia Mayweather 'Porini kuna mfalme mmoja tu'.
  Na katika majibu yake, Mayweather amemuonya Nurmagomedov kuwa na nidhamu kwenye pambano, kufuatia Mrusi huyo kuruka nje ya ulingo wakati wa pambano na McGregor na kwendaa kupigana na mmoja wa wafuasi wa mpinzani wake, jambo ambalo lilikemewa na Tume ya Michezo ya Jimbo la Nevada.

  Khabib Nurmagomedov alimpiga Conor McGregor wiki mbili zilizopita

  Mayweather amesema: "Vegas ni jiji la mapambano na baada ya pambano inabidi uitulize nafsi yako kama mwanamichezo kitaaluma, siyo tu ulingoni, bali hata nje ya ulingo,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYWEATHER AKUBALI KUPIGANA NA KHABIB, AMUONYA AWE NA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top