• HABARI MPYA

    Monday, January 23, 2017

    GABON WAWEKA REKODI YA WENYEJI KUTOLEWA MAPEMA AFCON

    HUZUNI kwa wenyeji, Gabon baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kufuatia sare ya bila kufungana na Cameroon mjini Libreville.
    Nyota Pierre-Emerick Aubameyang alikosa bao la wazi mapema tu wakati Denis Bouanga aliaanguka chini na kuangua kilio baada ya kugongesha nguzo dakika za mwishoni, hiyo ikiwa sare ya tatu mfululizo katika mechi zao nyingi.
    Na kwa sare hiyo pamoja na zile mbili za 1-1 dhidi ya Burkina Faso na Guinea-Bissau katika mechi za awali, Gabon inamaliza na pointi tatu na inaaga mashindano, wakiweka rekodi ya kuwa wenyeji wa nne na wa kwanza tangu Tunisia mwaka 1994 kutolewa hatua ya makundi.
    Pierre-Emerick Aubameyang akisikitika jana baada ya kukosa bao la wazi mapema tu

    Kwa pointi saba, Cameroon wanakwenda Robo Fainali kama vinara wa Kundi A wakifuatiwa na Burkina Faso ambayo jana iliifunga 2-0 Guinea-Bissau mjini Franceville.
    Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi B, Zimbabwe ya Bruce Kangwa wa Azam FC ikimenyana na Tunisia Uwanja wa d'Angondje na Senegal ikimenyana na Algeria Uwanja wa Franceville mechi zote zikianza Saa 4:00 usiku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GABON WAWEKA REKODI YA WENYEJI KUTOLEWA MAPEMA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top