• HABARI MPYA

  Thursday, February 18, 2016

  SIMBA WATUA DAR USIKU TAYARI ‘KUTAFUNA KANDAMBILI’ JUMAMOSI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  SIMBA SC imeondoka Morogoro baada ya mazoezi ya leo jioni kurejea Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu, Yanga SC.
  Watani hao wa jadi, wanatarajiwa kumenyana keshokutwa katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huo ukiwa mchezo wa marudiano, baada ya mchezo wa kwanza Septemba mwaka jana, Yanga kushinda 2-0.
  Simba SC iliweka kambi Morogoro tangu Jumatatu baada ya kushinda michezo miwili mfululizo mjini Shinyanga dhidi ya Kagera Sugar 1-0 na dhidi ya Stand United 2-1 Uwanja wa Kambarage.

  Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kufikia katika hoteli moja ya nyota tano katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ambako wachezaji watapumzika kabla ya mchezo wa Jumamosi.
  Wapinzani wao, wako Pemba tangu Jumapili baada ya kuwasili Mauritius, ambako walishinda 1-0 dhidi ya wenyeji Cerle de Joachim katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Na Yanga pia wanatarajiwa kuwasili kesho mchana Dar es Salaam, wao pia wakiwa na mpango wa kufikia katika hoteli moja ya nyota tano katikati ya Jiji. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WATUA DAR USIKU TAYARI ‘KUTAFUNA KANDAMBILI’ JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top