• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2016

  PHIRI AAHIDI KULIADABISHA TOTO LA YANGA SC KESHO SOKOIE

  Na Gwamaka Mwankota, MBEYA
  KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kwamba licha ya kuwa na majeruhi watatu kikosini, hana shaka yoyote na vijana wake kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara  dhidi ya Toto Africans ya Mwanza kwenye uwanja wa Sokoine hapo kesho.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, Phiri amesema kuwa ni wazi kesho City itawakosa mlinda lango Hanington Kalyesubula aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu jijini Dar es Salaam na beki Deo Julius aliyepata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons, huku pia kukiwa na hatihati ya kucheza kwa mlinzi Hassan Mwasapili.
  Kocha Phiri akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Mbeya

  “Nimepata ripoti ya daktari leo, imenishtua kidogo kuona tuna majeruhi watatu kwenye nafasi muhimu, baada ya mazoezi leo asubuhi nimegundua hakuna shaka yoyote juu ya hili, nina nyota wengi wanaoweza kucheza vizuri maeneo hayo, utakuwa ni mchezo mgumu hapo kesho, ila tutapambana kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwa sababu hivi sasa tunahitaji pointi tatu kwenye kila mchezo” alisema.
  Kuhusu mbinu gani atatumia hapo kesho kuikabili Toto Africans, ambayo tawi la Yanga SC mjini Mwanza, Kocha Phiri amesema si jambo jema sana kuweka hadharani mbinu zake hasa anakwenda kucheza mchezo muhimu lakini amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao na wategemee kuiona City ya tofauti na wanavyoijua.
  “Sidhani kama ni sahihi kusema juu ya mbinu  au aina ya mchezo hapa, kikubwa mashabiki waje uwanjani kwa wingi kuisapoti timu na wategemee ujio mpya  wa kikosi kiuchezaji uwanjani” alimaliza kusema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI AAHIDI KULIADABISHA TOTO LA YANGA SC KESHO SOKOIE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top