• HABARI MPYA

  Friday, February 19, 2016

  MAYANJA APANGUA KIKOSI SIMBA BAADA YA STRAIKA ALIYETAKA KUMUANZISHA KUUMIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Simba SC, Mganda Jackson Mayanja amemuodoa katika mipango yake ya mechi ya kesho, mshambuliaji chipukizi, Hajji Ugando baada ya kuumia jana mazoezini mjini Morogoro.
  “Hajji Ugando ameumia na kocha alitaka kumuanzisha, lakini sasa atalazimika kupanga mtu mwingine,”kimesema chanzo kutoka kambi ya Simba SC jana.
  Simba SC ilirejea Dar es Salaam jana usiku kwa basi kutoka Morogoro ilipokuwa imeweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Huo utakuwa mchezo wa marudiano, baada ya mchezo wa kwanza Septemba mwaka jana, Yanga kushinda 2-0, mabao ya Amissi Tambwe na Malimi Busungu.
  Hajji Ugando (kushoto) ameumia jana mazoezini mjini Morogoro hivyo hatacheza kesho  

  Simba SC iliweka kambi Morogoro tangu Jumatatu baada ya kushinda michezo miwili mfululizo mjini Shinyanga dhidi ya Kagera Sugar 1-0 na dhidi ya Stand United 2-1 Uwanja wa Kambarage.
  Kikosi cha Simba SC kimefikia katika hoteli moja ya nyota tano katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ambako wachezaji watapumzika kabla ya mchezo wa kesho.
  Wapinzani wao, Yanga walikuwa Pemba tangu Jumapili baada ya kuwasili wakitokea Mauritius, ambako walishinda 1-0 dhidi ya wenyeji Cercle de Joachim katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Na Yanga pia wamerejea leo mchana Dar es Salaam, wao pia wafikia katika hoteli moja ya nyota tano katikati ya Jiji. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYANJA APANGUA KIKOSI SIMBA BAADA YA STRAIKA ALIYETAKA KUMUANZISHA KUUMIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top