• HABARI MPYA

  Friday, February 19, 2016

  STRAIKA WA UGANDA FARUK MIYA ATUA STANDARD LIEGE KWA DOLA 400,000

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Farouk Miya leo ametambulishwa na vigogo wa Ligi Ku ya Ubelgiji, Standard Liege baada ya kuwasili kujiunga nayo.
  Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Vipers SC wamemuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 mwishoni mwa January mwaka kwa dau la dola za Kimarekani 400 000.
  Faruk Miya (kulia) akikabidhiwa jezi namba 15 leo Standard Liege
   

  Nyota huyo chipukizi amecheza mechi 49 na kufunga mabao 20 tangu ahitimu chuo cha St Mary’s Kitende mwaka 2013.
  Liege kwa sasa inashika nafasi ya nane katika Ligi ya timu 16, ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 26. 
  Miya alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Uganda mwaka 2015 baada ya kutoa mchango mkubwa kwa klabu yake kutwaa ubingwa wa ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STRAIKA WA UGANDA FARUK MIYA ATUA STANDARD LIEGE KWA DOLA 400,000 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top