• HABARI MPYA

    Thursday, July 10, 2014

    VAN GAAL ASEMA; "HUYU KIPA WA ARGENTINA NIMEMFUNDISHA MWENYEWE KUCHEZA PENALTI"

    KOCHA Louis van Gaal amesema kwamba alimfundisha Sergio Romero namna ya kuokoa penalti wakati alipokuwa anamfundisha kipa huyo wa Argentina katika klabu ya AZ Alkmaar.
    Romero alikuwa shujaa wa Argentina, wakati La Albiceleste inaifunga Uholanzi kwa penalti 4-2 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia mjini Sao Paulo baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 akiokoa penalti za Ron Vlaar na Wesley Sneijder.
    Argentina itamenyana na Ujerumani mjini Rio de Janeiro Jumapili, ikimtegemea zaidi Romero katika kampeni za ubingwa.
    Shujaa: Romero akishereheka baada ya Argentina kuitoa Uholanzi kwa penalti 4-2 janaComing back to haunt him: Van Gaal claims to have taught Romero how to save penalties
    Amemrudi kocha wake: Van Gaal amesema alimfundisha Romero kuokoa penalti

    Msimu uliopita kipa huyo alicheza kwa Monaco akitokea klabu yake, Sampdoria, aliyojiunga nayo mwaka  2011.
    Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa mbali kabisa na chaguo la kwanza msimu uliopita kwa utaratibu wa klabu hiyo.
    Hakika, kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal alikuwa anamjua vizuri Romero kabla ya Kombe la Dunia kwa sababu alifanya nays kazi Ligi Kuu ya Uholanzi, maarufu kama Eredevisie mwaka 2009 katika klabu ya AZ Alkmaar. Jana amemkatili kocha wake aliyemfundisha kuzuia penalti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VAN GAAL ASEMA; "HUYU KIPA WA ARGENTINA NIMEMFUNDISHA MWENYEWE KUCHEZA PENALTI" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top