SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeisimamisha Nigeria kushiriki mashindano yote ya soka, baada ya Moafisa wa Serikali kuwatimua viongozi wa Shirikisho la soka Nigeria (NFF).
Hii inamaanisha- Nigeria sasa haitashiriki mashindano yoyote, iwe ya ngazi ya klabu au kimataifa.
FIFA iliionya Nigeria mapema kwamba ingeichukulia hatua hiyo ifikiapo Jumanne, kama viongozi wa NFF hawatakuwa wamerejeshewa madaraka yao, lakini Serikali ikapuuza makatwa hayo.
Mwishoni mwa wiki, Serikali ya Nigeria iliteua Kamati kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi huru na wa haki utakapofanyika kwa mwongozo wa Wizara ya michezo.
FIFA katika taarifa yake, imesema adhabu hiyo itaondolewa tu iwapo uongozi wa waliochaguliwa na inaowatambua watarejeshwa madarakani.
Adhabu hiyo itaiathiri timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Super Eaglets ambayo imefuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia iwapo itakuwa inaendelea hadi Julai 15.
Hata hivyo, Msemaji wa Serikali amesema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata Mwenyekiti wa shirikisho hilo la soka, Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.
Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo mabaya kwenye Kombe la Dunia huko Brazil.
Wajumbe wa NFF waliafiki uamuzi wa Mahakama ya kumn'goa Mwenyekiti huyo madarakani, lakini lakini kwa sasa Serikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma taarifa za mkutano maalum uliofanyika na Wajumbe wa NFF kuhudhuria.
Mabingwa hao wa Afrika, walitoilewa katika Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia na Ufaransa, hiyo ikiwa
mara ya tatu Super Eagles kutinga hatua ya mtoano baada ya awali kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.

.png)
0 comments:
Post a Comment