• HABARI MPYA

    Thursday, July 17, 2014

    UMAFIA HADI ULAYA, CHELSEA YAIPINDUA ARSENAL DILI LA KHEDIRA

    KLABU ya Chelsea ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsaini Sami Khedira baada ya jana usiku wakala wake kusema hakuna makubaliano yaliyofikiwa na Arsenal.
    Kocha wa Blues, Jose Mourinho amemsajili beki wa kushoto Filipe Luis kutoka Atletico Madrid kwa Pauni Milioni 18 na kuhamishia nguvu zake kwa kiungo wa Ujerumani, Khedira.
    Ilikuwa inafahamika Arsenal ilikubali kutoa Pauni Milioni 20 kwa Real Madrid kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini walikuwa wanasuasua kufika kiwango cha mshahara anaotaka, Pauni 180,000 kwa wiki.
    Yuko safarini: Sami Khedira hajasaini mkataba mpya Real Madrid na anajiandaa kuondoka

    Pamoja na hayo, wakala wa Khedira, Jorg Neubauer amesema: "Hatupo katika mazungumzo na Arsenal. Sifikiri wanweza kukubaliana ada, vinginevyo ningeambiwa,". 
    Khedira anavutiwa na Mourinho tangu anafundisha Real na kocha huyo inafahamika pia anampenda sana mchezaji huyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UMAFIA HADI ULAYA, CHELSEA YAIPINDUA ARSENAL DILI LA KHEDIRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top