• HABARI MPYA

    Thursday, July 17, 2014

    MOMBEKI BYE- BYE SIMBA SC, ATUA JKT RUVU YA MINZIRO NA KUANZA KAZI MARA MOJA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Betram Mombeki amejiunga na JKT Ruvu Stars ya Pwani- maana yake ameijiondoa Simba SC.
    Pamoja na kuonyesha uwezo wa kuridhisha akiwa Simba SC msimu uliopita, lakini Mombeki alijikuta katika wakati mgumu mbele ya kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic.
    Loga alikuwa akimuacha benchi Mombeki, na hata alipoamua kumuingiza, wakati mwingine alimtoa katika mechi baada ya kufanya kosa kidogo, jambo ambalo wazi limemkera mshambuliaji huyo mwenye nguvu na ameamua kwenda kujaribu maisha mapya.
    Betram Mombeki katika jezi ya JKT Ruvu leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

    Mombeki mwenyewe hakutaka kuzungumza mengi zaidi ya kusema; “Ndiyo, nipo hapa sasa, naangalia ustaarabu mpya,”. 
    Meneja wa JKT Ruvu Stars, Suleiman Oga amesema wamempokea Mombeki na wapo katika mazungumzo naye kwa ajili ya kumsajili.
    Kocha Freddy Felix Minziro leo amempanga Mombeki JKT Ruvu ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mombeki nyuma ya kiungo wa Azam FC, Bryson Raphael leo Chamazi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOMBEKI BYE- BYE SIMBA SC, ATUA JKT RUVU YA MINZIRO NA KUANZA KAZI MARA MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top