• HABARI MPYA

    Friday, July 18, 2014

    MSHAMBULIAJI WA SUNDERLAND ALIYEKUWA AKILIPWA PAUNI 10,000 KWA WIKI SASA ANAHUDUMIA KWENYE MELI KWA MALIPO YA PAUNI 400 KWA WIKI

    STRAIKA wa zamani wa Sunderland na timu ya taifa ya Uskochi, Kevin Kyle  amekuwa akikidhi mahitaji ya familia yake kwa kufanya kazi kama mtunza stoo katika meli moja kwenye visiwa vya Shetland.
    Kyle, ambaye amewahi kucheza mechi 10 kwenye timu ya taifa ya nchi yake, aliachana na klabu yake ya mwisho ya Ayr United mapema mwaka huu na kwa sasa anafanya kazi masaa 12 katika meli ya Regina Baltica huko Lerwick.
    Meli hiyo inatumika kwa hoteli inayoelea kwenye maji kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye viwanda vya mafuta kwa mujibu wa rekodi za kila siku Kyle anafanya kazi ya kusafisha meli hiyo, kutandika vitanda na kuweka vitu stoo.

    Mfanyakazi was too: Kyle akihamisha baadhi ya chupa za maji kama sehemu ya kazi yake Regina Baltica
    Target man: 6ft 3in Kyle was renowned for his hold-up play and aerial ability in his prime
    Target man: 6ft 3in Kyle was renowned for his hold-up play and aerial ability in his prime
    Straika:  Akiwa na urefu wa futi 6 na inch 3, Kyle alikuwa akisifika kwa kucheza mipira ya vichwa 
    Hard graft: Kevin Kyle celebrates scoring for Sunderland back in May 2004
    Furaha: Kevin Kyle akishangilia baada ya kufunga bao akiwa na kikosi cha Sunderland, Mei 2004

    Alipoulizwa na Daily Record kuhusu kazi yake  inayomuingizia pauni 800 kwa wiki mbili, Kyle mwenye umri wa miaka 33 alisema; “Najaribu kuikimu familia yangu.”
    Kyle alianza kucheza soka katika klabu ya Sunderland mwaka 2000, ambako aliichezea katika mechi 39 za Ligi Kuu England na kufunga mara moja.
    Aliichezea Uskochi mechi yake ya kwanza mwaka 2002 na kuifungia nchi yake mara moja.
    Aliichezea klabu za Coventry (ilimlipia pauni 600,000 kutoka Sunderland mwaka 2006), Kilmarnock, Hearts na Rangers pamoja na timu kadhaa zingine kwa mkopo kabla ya kuhamia Ayr United, ambako mara ya mwisho alichezea Januari.
    Kyle bado hajatundika daluga rasmi, lakini amekosa klabu ya kuchezea tangu aondoke Ayr United.
    Mzaliwa huyo wa Stranraer ambaye zamani ameathiriwa na matatizo ya kucheza kamari, kiasi cha kutumia pauni 7,000 kwa wiki kwenye kamari. Amekuwa akitumia muda wake wa ziada kuwaambia wachezaji vijana athari za kuendekeza kucheza kamari.
    Kwenye kilele cha mafanikio yake ya soka Kyle alikuwa akilipwa pauni 10,000 kwa wiki yaani kwa siku aliingiza fedha nyingi kuliko zile ambazo anangiza sasa kwa wiki mbili.
    Out of contract: Kyle has not officially retired from football but has been without a club since January
    Out of contract: Kyle has not officially retired from football but has been without a club since January
    Hana mkataba: Kyle hajatundika daluga rasmi kutoka kwenye soka lakini amekuwa hana timu tangu Januari
    International honours: Kyle rises for a header playing for Scotland against Denmark in August 2002
    Heshima ya kimataifa: Kyle akiruka kichwa wakati akiichezea Scotland dhidi ya Denmark, Agosti 2002
    Injury problems: Kyle's two years at Hearts from 2010 to 2012 were beset by injuries
    Tatizo la Majeruhi: Miaka miwili ya  Kyle katika klabu ya Hearts kati ya 2010 hadi 2012 ilitawaliwa na majeruhi

    WASIFU WA KEVIN KYLE:

    Sunderland (2000-06), Huddersfield (2000)*, Darlington (2000-01)*, Rochdale (2001)*, Coventry (2006-09), Wolves (2008)*, Hartlepool (2008)*, Kilmarnock (2009-10), Hearts (2010-12), Rangers (2012-13), Ayr United (2013-14). Scotland (2002-10)
    Jumla: Mechi 320, mabao 69.
    * Inahusiaha timu alizocheza kwa mkopo
    Kyle alicheza kwa kipindi kifupi Rangers katika msimu wa 2012-13 na anakiri kushtushwa na fedha ambazo wachezaji walikuwa wakipata kwenye klabu hiyo ambayo ilikuwa na matatizo ya fedha.
    Alisema: “Kuna wachezaji pale Rangers ambao hawawezi kuamini jinsi gani wanabahati kwa kile wanachokiingiza.
    “Nilimuuliza mchezaji mwenzangu wakati wa kiangazi, ‘Kweli Rangers wamekupa ofa ya kiasi hicho cha fedha?”
    “Alinijibu, “Unajua nini? Nadhani ninaweza kuwakamua zaidi.”
    Brief stay: Kyle scores three goals in 11 games in all competitions in for Rangers
    Kwa muda tu: Kyle alifunga mabao matatu katika mechi 11 za mashindano yote za Rangers
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSHAMBULIAJI WA SUNDERLAND ALIYEKUWA AKILIPWA PAUNI 10,000 KWA WIKI SASA ANAHUDUMIA KWENYE MELI KWA MALIPO YA PAUNI 400 KWA WIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top