• HABARI MPYA

    Thursday, July 17, 2014

    KAVUMBAGU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM, KIPRE TCHETCHE KAMA KAWA, AZAM YAIKALISHA TIMU YA MINZIRO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    AZAM FC imeshinda mechi ya tatu mfululizo ya kirafiki, baada ya kuilaza mabao 2-1 JKT Ruvu Stars Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wachezaji wa kigeni wakiendelea kuibeba timu.
    Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, walikwenda kupumzika wakiwa tayari wanaongoza tayari kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast.
    Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbangu akimiliki mpira mbele ya beki wa JKT Ruvu, Mohammed Fakhi leo Chamazi
    Mshambuliaji wa Azam Lionel Saint- Preux akipasua katikati ya mabeki wa JKT Ruvu, Fakhi kulia na Nafo Sasane kushoto
    Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akimtoka beki wa JKT Ruvu, Haruna Shamte
    Kiungo wa Azam FC, Bryson Raphael akifumua shuti pembeni ya Hassan Bilal wa JKT Ruvu
    Beki chipukizi wa Azam FC, Abdul Mgaya akiondosha mpira mbele ya mshambuliaji wa JKT Ruvu, Betram Mombeki
    Kipindi cha pili, kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alibadilisha karibu wachezaji wote walioanza na JKT Ruvu ya Freddy Felix Minziro ilitumia mwanya huo kujipatia bao la kusawazisha lililofungwa na Hassan Bilal, aliyemalizia kazi nzuri ya Betram Mombeki.
    Mshambuliaji mpya wa Azam FC kutoka Haiti, Leonel Saint- Preux alicheza vizuri na ndiye aliyetoa pasi ya bao la pili, wakati Ismaila Diara kutoka Mali alikuwa jukwaani kabisa kutokana na mejeruhi.
    Didier Kavumbangu akipiga mpira mbele ya beki wa JKT Ruvu, Mohammed Fakhi
    Katibu wa Azam FC, Nassor Iddirsa kulia akiangalia muda wakati mchezo huo ukielekea ukingoni
    Chipukizi waliopandishwa kutoka akademi, Abdul Mgaya, Bryson Raphael, Malik Farid, Dizana Issa na Mudathir Yahya ambao walianza kipindi cha kwanza, wote walicheza vizuri.
    Awali, Azam FC ilizifunga kombaini ya Jeshi 3-2, mabao yake yakifungwa Ismaila Diara mawili na Mudathir Yahya moja, kabla ya kuilaza Polisi Morogoro 1-0, bao pekee la Leonel Saint- Preux.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAVUMBAGU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM, KIPRE TCHETCHE KAMA KAWA, AZAM YAIKALISHA TIMU YA MINZIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top