• HABARI MPYA

    Friday, July 04, 2014

    KAGERA SUGAR WAINGIA KAMBINI ALHAMISI KUANZA KUKUSANYA PUMZI ZA UBINGWA LIGI KUU 2015

    Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Kagera Sugar kitaingia kambini mkoani Kagera Alhamisi kuanza maandalizi ya msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), imefahamika.
    Mrage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar, ameiambia BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam kwamba timu yao itaingia rasmi kambini Julai 10 (Alhamisi) kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu huo Agosti 24 mwaka huu.
    "Tunaingia kambini tukiwa tumefanya usajili wa nguvu ingawa kuna nafasi moja ya mshambuliaji bado hatujapata mtu sahihi," amesema.
    Kikosi cha Kagera Sugar kinaingia kambini Alhamisi

    'THEMI FELIX PIGO'
    Aidha, Kabange amesema kuondoka kwa mshambuliaji Themi Felix ni pigo kwa mabingwa hao wa Kombe la Tusker 2004.
    "Kusema kweli Themi ni pigo kwetu lakini lazima tukumbuke kwamba soka ni biashara na wachezaji wanaangalia maslahi yao. Tulijitahidi sana kumbakisha lakini ikashindikana," amesema Kabange.
    "Pengo lake tunaamini litazibwa na wachezaji chipukizi ambao kwa sasa hatuwezi kuwaanika kwa majina," amesema zaidi kocha huyo.
    Themi Felix kulia amehamia Mbeya City

    Felix alijiunga na kikosi cha kocha Juma Mwambusi cha Mbeya City baada ya kumalizika kwa msimu wa 2013/14 wa VPL.
    Kagera Sugar inayonolewa na Mganda Jackson Mayanja ilimaliza katika nafasi ya tano ya msimamo wa VPL msimu wa 2013/14 ikiwa na pointi 38, sawa na Simba walioshika nafasi ya nne na Ruvu Shooting waliokamata nafasi ya sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR WAINGIA KAMBINI ALHAMISI KUANZA KUKUSANYA PUMZI ZA UBINGWA LIGI KUU 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top