• HABARI MPYA

    Sunday, July 06, 2014

    DI MARIA AAGA KOMBE LA DUNIA ARGENTINA IKITINGA NUSU FAINALI

    MSHAMBULIAJI wa Argentina, Angel Di Maria anatarajiwa kukosa mechi zilizonaki za timu yake za Kombe la Dunia baada ya kuumia jana katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Ubelgiji mjini Brasilia.
    Di Maria atakwenda kufanyiwa vipimo baada ya kuumia dakika ya 33 jana, huku vyombo vya Habari Amerika Kusini vikiripoti kwamba mchezaji huyo wa Real Madrid ndiyo ameaga Kombe la Dunia.
    Argentina ilitinga Nusu Fainali yake ya kwanza ya Kombe kla Dunia tangu mwaja 1990, lakini Di Maria hakushangilia ushindi na wenzake baada ya kuumia na kutoka kipindi cha kwanza.
    Shakanni: Angel Di Maria aliumia dhidi ya Ubelgiji jana
    Replaced: Di Maria was substituted in the 33rd-minute with a thigh injury in Argentina's 1-0 win over Belgium
    Alitoka: Di Maria alimpisha Enzo Perez dakika ya 33

    Enzo Perez aliingia kuchukua nafasi ya Di Maria, ambaye alifunga bao pekee katika ushindi wa Argentina wa 1-0 mchezo wa 16 Bora dhidi ya Uswisi.
    Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella amethibitisha wing huyo wa Real Madrid atafanyiwa vipimo leo. Argentina itamenyana na Uholanzi katika Nusu Fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MARIA AAGA KOMBE LA DUNIA ARGENTINA IKITINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top