• HABARI MPYA

    Monday, July 07, 2014

    STARS YAREJEA DAR, YAENDA MBEYA KESHO KWA MAANDALIZI YA MWISHO KABLA YA MECHI NA MSUMBIJI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimerejea usiku wa jana mjini Dar es Salaam kesho kutoka Gaborone, Botswana kilipokuwa kimeweka kambi ya wiki mbili.
    Baada ya kuwasili Dar es Salaam majira ya saa moja na ushei usiku, wachezaji wa Stars walikwenda katika hoteli ya Acommondia kwa mapumziko ya siku moja kabla ya kwenda kuendelea na kambi mjini Mbeya.
    Stars itaondoka tena kesho Dar es Salaam kwa ndege kwenda Mbeya kuweka kambi ya mwisho kabla ya mechi na Msumbiji.
    Mrisho Ngassa kushoto ataingia kambini leo Taifa Stars 

    Timu hiyo inayofundishwa na kocha Mholanzi, Mart Nooij iliweka kambi Botswana kujiandaa mchezo dhidi ya Msumbiji ‘Mambas’, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco.    
    Taifa Stars na Mambas zitamenyana nyumbani na ugenini katika Raundi ya Pili kuwania kupangwa katika makundi ya kufuzu AFCON mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Stars pamoja na kujifua vikali, ikiwa huko ilipata pia mchezo mmoja wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Botswana na kufungwa mabao 4-2.
    Mshambuliaji Mrisho Ngassa ambaye alikuwa Afrika Kusini kufanya mipango ya kujjiunga na klabu ya Free State Stars ya huko, anatarajiwa kuungana na kikosi cha Nooij katika leo Dar es Salaam.
    Pamoja na Ngassa kufikia makubaliano na Free State, lakini biashara ilishindikana baada ya klabu yake Yanga SC kudai dau kubwa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS YAREJEA DAR, YAENDA MBEYA KESHO KWA MAANDALIZI YA MWISHO KABLA YA MECHI NA MSUMBIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top