• HABARI MPYA

    Thursday, July 10, 2014

    BREAKING NEWS; CASSILAS WA MTIBWA SUGAR ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIPA wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba SC ya Dar es Salaam.
    Kipa huyo ambaye mara kadhaa huitwa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesaini leo Dar es Salaam mbele ya viongozi wa Simba SC.
    Kipa huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara amekuwa akiibeba Mtibwa Sugar kwa misimu mitatu iliyopita, tangu kuondoka kwa Shaaban Hassan Kado.
    Cassillas akisaini pembeni ya Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Said Tuliy
    Kipa huyo ambaye mara kadhaa huitwa timu ya taifra, Taifa Stars amesaini leo Dar es Salaam mbele ya viongozi wa Simba SC.
    Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Said Tuliy kushoto akiwa na Cassilas baada ya kusaini leo

    Cassilas anayeishi Mji Mwema, Kigamboni mjini Dar es Salaam anakwenda kufanya idadi ya makipa watatu Simba SC, ambao ni Ivo Mapunda na Abuu Hashim baada ya kutemwa kwa Mghana, Yaw Berko. 
    Maana yake, Cassilas sasa atalazimika kwenda kuchuana na kipa mkongwe Ivo, kugombea namba katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
    Cassilas ameonyesha uwezo wa kuridhisha akiwa Mtibwa Sugar, hususan katika mechi kubwa za Ligi Kuu dhidi ya miamba kama Simba, Yanga na Azam FC kwa kudaka kwa uhodari mkubwa. 
    Alikuwemo katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen lakini baada ya kuja kwa Mholanzi, Mart Nooij kinda huyo amepoteza nafasi kwenye timu hiyo.
    Upo uwezekano mkubwa Cassilas akarejeshwa Stars, iwapo atafanya vizuri Simba SC kwa sababu hakuna shaka ni milnda mango hodari na mwenye kipaji. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BREAKING NEWS; CASSILAS WA MTIBWA SUGAR ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top