• HABARI MPYA

    Wednesday, August 14, 2013

    WENGER SASA ATAKA KUMSAJILI MICHU IWAPO ATAMKOSA SUAREZ, ABISHA HODI NA BAYERN KUOMBA SAINI YA GUSTAVO

    IMEWEKWA AGOSTI 14, 2013 SAA 10:49 ALFAJIRI
    KLABU ya Arsenal imeibuka na mpango B katika msako wake wa mshambuliaji wa kati iwapo itamkosa Luis Suarez.
    The Gunners imemuweka nambari moja mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka Liverpool, lakini tayari ofa zao mbili zimekwishapigwa chini na klabu ya Anfield.
    Arsenal bado ina matumaini ya kushinda sakata hilo kwa kumnsa mpachika mabao huyo tishio, ikibidi kutuma ofa ya tatu ya Pauni Milioni 50, kiwango cha chini kinachotakiwa na Liverpool.
    Lean on me: Luis Suarez is training alone at Melwood after trying to force a move away from the club
    Niagalie: Luis Suarez anafanya mazoezi peke yake Melwood kama adhabu baada ya kulazimisha kuondoka
    Kupitia Sportsmail, BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba The Gunners imeanza mpango wa kumpata mkali mwingine, iwapo itamkosa Suarez.
    Majadiliano baina ya benchi la Ufundi na Maskauti wa klabu yamechukua nafasi siku chache zilizopita juu ya mchezaji mbadala.
    Tayari, Arsenal imewakosa Gonzalo Higuain na Stevan Jovetic ambao wote kocha Arsene Wenger alikuwa anawahitaji sana majira haya ya joto, hivyo akahamia kwa Suarez.
    Interested? Edin Dzeko, pictured in Munich with Manchester City, has found form in pre-season
    Anatakiwa? Edin Dzeko, pichani mjini Munich akiwa na Manchester City, amerudi katika kiwango kwenye mechi za kujiandaa na msimu
    Michu
    Stevan Jovetic
    Wengine wanaotakiwa: Stevan Jovetic (kulia) amechagua Manchester City, lakini Michu (kushoto) anabaki kwenye rada za Arsenal
    One that got away: Gonzalo Higuain (centre) left for Napoli. Here, he celebrates scoring against Benfica
    Mmoja aliyeota mbawa: Gonzalo Higuain (katikati) ametimkia Napoli. Hapa akishangilia kufunga dhidi ya Benfica
    Higuain ameenda Napoli na Jovetic ametua Manchester City, wakiiacha The Gunners ikisotea sani za wengine.
    Wayne Rooney alikuwa anatakiwa pia mwanzoni, wakati klabu hiyo imepokea taarifa ya Maskauti wake kuhusu mshambuliaji wa Swansea, Michu na wa Manchester City, Edin Dzeko.
    Liverpool wanasistiza hawatamuuza Suarez kwa Arsenal kwa namna yoyote, lakini The Gunners haijabwaga manyanga katika jaribio lake la kunasa saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye yu tayari kuondoka Anfield kutua Emirates.
    Mchezaji pekee ambaye Arsenal ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili ni kiungo mkabajia wa Bayern Munich, Luis Gustavo.
    The Gunners imeanza mazungumzo na mabingwa hao wa Ulaya juu ya ofa ya Pauni Milioni 14.5 kumnasa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil.
    Still searching: Arsene Wenger (right), talking to Manuel Pellegrini, is looking to add to his squad
    Bado anasaka: Arsene Wenger (kulia), akizungumza na Manuel Pellegrini, anataka kuongeza wachezaji kikosini mwake
    Na Gustavo, ambaye hana nafasi kwa sasa katika kikosi cha kwanza Allianz Arena, yupo tayari kuhamia London, na amesema: "Wao [Arsenal] ni timu kubwa na ambayo itakuwa ni nafasi kubwa.
    "Nataka kwenda klabu ambayo nitacheza,". Wakati huo huo, Malaga inataka kumtumia beki wa kulia, Jesus Gamez kama sehemu ya majadiliano ya kumsaini Nicklas Bendtner.
    Arsenal inataka kusaini beki mpya wa kulia awe msaidizi wa Bacary Sagna, ambaye anaweza kutumika katika beki ya kati mwanzoni mwa msimu kutokana na Thomas Vermaelen kuwa majeruhi.
    Na Malaga inataka kumtumia Gamez, mwenye umri wa miaka 28, kama sehemu ya dili lao na Gunners kwa Bendtner.
    Luiz Gustavo
    Nicklas Bendtner
    Anayetoka na Anayeingia: Luiz Gustavo (kushoto) anaweza kutua akitokea Bayern Munich wakati Nicklas Bendtner anataka kuondka
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WENGER SASA ATAKA KUMSAJILI MICHU IWAPO ATAMKOSA SUAREZ, ABISHA HODI NA BAYERN KUOMBA SAINI YA GUSTAVO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top