• HABARI MPYA

    Friday, August 23, 2013

    ARSENE WENGER SASA AMGEUKIA FLAMINI, AMREJESHA EMIRATES NA TAYARI KAANZA MAZOEZI BADO KUSAINI MKATABA TU

    IMEWEKWA AGOSTI 23, 2013 SAA 10:52 ALFAJIRI
    KOCHA Arsene Wenger yuko katika siku 12 ngumu za kukimbizana kukamilisha usajili kabla ya dirisha kufungwa na sasa amehamishia ndoana zake kwa Mathieu Flamini, kiasi cha miaka mitano tangu aondoke Arsenal kuhamia AC Milan.
    Klabu hiyo ya Italia imemtema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na sasa kiungo huyo kiasi cha wiki mbili amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Wenger.
    Kocha wa Arsenal amevutiwa kiasi cha kutosha na hali ya mchezaji huyo na yuko tayari kumpa ya Mkataba Flamini baada ya kukubali kurejea nyumbani licha ya kutakiwa na klabu nyingine.
    Mathieu Flamini
    Anarudi: Arsenal inajiandaa kumpa Mkataba Mathieu Flamini baada ya kutemwa AC Milan majira haya ya joto
    Mathieu Flamini
    Wameungana tena: Akiwa amiechezea zaidi ya mechi 100 The Gunners, Flamini aliondoka Arsenal kuhamia AC Milan mwaka 2008
    Atakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Wenger majira haya ya joto— wote wachezaji huru — na mchezaji wa nne wa zamani wa timu hiyo kusainiwa tena na kocha huyo, baada ya awali kuwarejesha Sol Campbell, Jens Lehmann na Thierry Henry Emirates.
    Wenger anatumai dili hilo litafuatiwa na usajili wa mchezaji mqwenye jina kubwa katika klabu hiyo.
    Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ni mchezaji anayetakiwa zaidi kwa sasa na Wenger baada ya kushindwa kuwapata Luis Suarez au Wayne Rooney.
    Na Mfaransa huyo pia ametenga dau kubwa zaidi kwa ajili ya mchezaji mwenzake Benzema, Angel Di Maria, na pia atarajea na ofa nzuri zaidi kwa ajili ya kiungo wa Newcastle Yohan Cabaye na kipa wa Valencia, Vicente Guaita.
    Mchezajhi mmoja tu ambaye anaweza kuondoka kwa sasa ni Lukas Podolski, ambaye anatakiwa na Schalke.
    Thierry Henry
    Kijana wa zamani wa Arsenal: Thierry Henry alitangaza kurejea klabu hiyo na kufunga bao katika Kombe la FA dhidi ya Leeds mwaka 2012
    Jens Lehmann
    Sol Campbell
    Jens Lehmann na Sol Campbell pia walijiunga tena na timu ya Arsene Wenger baada ya kuhama
    Real itataka dau la jumla la Pauni Milioni 60 ili kuwauza wote Benzema na Di Maria. Newcastle inataka angalau Pauni Milioni 20 kwa Cabaye, wakati Guaita imeelezwa ni kiasi cha Pauni Milioni 25.6 kuvunja Mkataba wake.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENE WENGER SASA AMGEUKIA FLAMINI, AMREJESHA EMIRATES NA TAYARI KAANZA MAZOEZI BADO KUSAINI MKATABA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top