IMEWEKWA AGOSTI 24, 2013 SAA 2:27 USIKU
MSHAMBULIAJI Lukas Podolski amefunga mabao mawili wakati Arsenal ikipata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua Fulham 3-1 kwenye Uwanja wa Craven Cottage.
Podolski alifunga mabao hayo katika dakika za 41 na 68, wakati bao lingine la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud dakika ya 14 na bao la kufutia machozi la Fulham lilifungwa na Darren Bent dakika ya 77.
Kikosi cha Arsenal leo kilikuwa: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs, Ramsey, Rosicky/Wilshere dk70, Cazorla, Podolski/Sanogo dk81, Walcott, Giroud/Monreal dk72.
Fulham: Stockdale, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Duff/Bent dk59, Parker, Sidwell/Karagounis dk75, Taarabt/Kacaniklic dk62, Kasami na Berbatov.

Safi: Arsenal wakishangilia ushindi dhidi ya Fulham leo

Imetulia: Olivier Giroud akifunga la kwanza

La pili: Lukas Podolski akiifunia la pili Arsenal

Mwanasoka wa kimataifa wa Ujerumani akishangilia na Giroud baada ya kufunga la tatu

La kufuta machozi: Darren Bent akiondoka na mpira baada ya kufunga

Anguka na teleza: Santi Cazorla na Adel Taarabt wakipambana

Mbio: Pajtim Kasami na Per Mertesacker wakikimbilia mpira

Kazi: Taarabt alifanya kazi kubwa kwa Fulham leo

Scott Parker ameanza maisha mapya Fulham, ambayo ni klabu yake ya tano London

Kiulaini: Theo Walcott akimiliki mpira pembeni ya Steve Sidwell

Akaribishwa na kipigo: Mwenyekiti mpya wa Fulham, Shahid Khan akiwasalimia mashabiki


.png)