IMEWEKWA AGOSTI 23, 2013 SAA 11:06 ALFAJIRI
BORA kwako kucheza kwenye Uwanja usio na mashabiki wa kutosha Tbilisi, au kuhamia Bernabeu Madrid?
Unataka kucheza Ligi ya Mabingwa au Europa League? Usiku wa Jumatano katika ITV1 au Alhamisi usiku katika ITV4? Huna akili, sawa?
Hiyo ndiyo picha ya Gareth Bale mjini London Alhamisi usiku, akiangalia wachezaji wenzake kwenye TV wakicheza mechi ya kwanza ya Europa League kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la UEFA ndogo dhidi ya Dinamo Tbilisi.
Dinamo Tbilisi: Loria, Khurtsilava, Giorgi Gvelesiani, Kvaratskhelia, Glisic (Papava 46), Grigalashvili, Dzaria, Kvirkvelia, Merebashvilli, Xisco (Vouho 42), Dvali.
Katika mchezo huo, ilishinda 5-0, mabao yake yakiwekwa nyavuni na Townsend dakika ya 12, Paulinho dakika ya 44, Soldado dakika ya 58 na 67 na Rose dakika ya 64.
Kikosi cha Spurs jana kilikuwa: Lloris, Naughton, Dawson, Kaboul, Rose, Paulinho/Carroll dk71, Dembele, Capoue, Sigurdsson/Chadli dk61, Townsend, Soldado/Kane dk71.

Mawili nyavuni: Roberto Soldado (kushoto) alifunga mawili na Paulinho alifunga pia

Mtu wa raha: Andros Townsend (kulia) akishangilia na Soldado

Soldado akiifungia bao la tatu Spurs

Danny Rose akifunga

Soldado akimtungua Nacer Chadli kwa krosi ya Loria

Jezi nyeupe zinang'ara: Spurs wakishangilia bai la Rose

Anabinuka: Paulinho anabinuka kupiga mpira mbele ya mchezaji wa Dinamo kwenye boksi


.png)