IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 12:32 ASUBUHI
KOCHA Jose Mourinho ameendelea kutamba katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa.
Kwanza, kocha huyo wa Chelsea alitikiswa kwa bao la kusawazisha la Christian Benteke na kisha akavaana na kocha wa Aston Villa, Paul Lambert.
Mourinho anafahamu Chelsea ilibahatika. Wameshinda wakati Branislav Ivanovic, ambaye angepewa kadi nyekundu kiulaini kwa kumchezea rafu Benteke, kufunga bao la ushindi.
Luna alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya saba kabla ya Benteke kusawazisha dakika ya 45 na Ivanovic akafunga la ushindi dakika ya 73.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, Oscar/Van Ginkel dk84, Mata/Schurrle dk65, Hazard na Ba/Lukaku dk65.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Clark/Okore dk43, Luna, El Ahmadi/Tonev dk82, Westwood, Delph, Weimann, Benteke na Agbonlahor.
Gonga HAPA matokeo zaidi, msimamo na ratiba Ligi Kuu England
Pointi tatu: Chelsea wakishangilia baada ya kushinda 2-1 jana
Ivanovic akifunga bo la ushindi
Jose Mourinho akizinguana na kocha mpinzani wake, Paul Lambert
Hakuna furaha: Ugomzi ulitokana na rafu ya Ivanovic kwa Christian Benteke
Refa wa akiba akijaribu kuwasuluhisha
Lambert akijibu mapigo
Ivanovic akimchezea rafu Christian Benteke, lakini akapewa kadi ya njano tu
Benteke akishika uso wake baada ya rafu ya Ivanovic
Chelsea ilipata bao la mapema baada ya shutila Eden Hazard kumfanya Antonio Luna ajifunge.
Jinsi Luna alivyojifunga na kuipa Chelsea pointi tatu- gonga kupata zaidi yaliyojiri Stamford Bridge
Benteke akishangilia bao lake
Kocha wa Villa, Lambert akiruka kushangilia bao la Benteke
Demba Ba akipambana na Jores Okore
Eden Hazard alitoa mchango mkubwa kwa bao la kwanza la Chelsea
Beki wa Villa, Demba Ba akipambana kabla ya kutolewa
Ciaran Clark akitokwa damu
Ramires na Fabian Delph wakipambana