IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 6:47 USIKU
MSHAMBULIAJI anayetakiwa na Arsenal, Karim Benzema ameiongoza timu yake kushinda mechi ya pili ya La Liga baada ya usiku huu kufunga bao pekee katika ushindi wa Real Madrid wa 1-0 dhidi ya Granada.
Mfaransa huyo alimtungua kipa wa wenyeji, Roberto Fernandez dakika ya 10, baada ya kupata pasi ya Cristiano Ronaldo akiwa kwenye boksi.
Wakati huo huo, kipa Iker Casillas, nyota mwingine wa Madrid anayetakiwa na kocha wa Gunners, Arsene Wenger, ameendelea kusota benchi.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego López; Arbeloa, Sergio Ramos, Pepe, Marcelo/Nacho, Modric, Ozil/Casemiro, Di María/Carvajal, Isco, Ronaldo na Benzema.
Granada: Roberto; Nyom, Diakhaté, Mainz, Angulo; Iturra, Yebda/Fran Rico, Brahimi, Benítez/Buonanotte, Piti na El Arabi/Riki.
Kitu nyavuni! Karim Benzema akifumua shuti kumfunga kipa wa Granada, Roberto Fernandez
Wote tabasamu: Karim Benzema akipongezwa na Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao lake la pili la msimu
Benchi na yeye: Kipa Iker Casillas anayetakiwa na Arsenal, ameendelea kusota benchi
Mchezaji mpya wa Real Madrid, Isco, aliyesajiliwa kutoka Malaga majira haya ya joto, akimtoka beki wa pembeni wa Granada, Allan Nyom
Kadaka: Kipa Fernandez akidaka
Usiku mzito: Fernadez akiokoa kona
Refaaa? Cristiano Ronaldo akililia mpira wa adhabu baada ya kuchezewa faulo