IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 11:46 ALFAJIRI
KLABU ya Barcelona imethibitisha Lionel Messi ameumia mguu wake wa kushoto katika mchezo wa jana usiku wakitoka sare ya 1-1 Atletico Madrid.
Nyota huyo wa Argentina alimpisha Cesc Fabregas kipindi cha pili katika mchezo wa kwanza wa Super ya Hispania kwenye Uwanja wa Vicente Calderon.
"Messi alitolewa nje kutokana na maumivu ya nyuma ya goti lake yaliyosababishwa na pigo,"imesema taarifa ya Barca.
Mshambuliaji wa zamani wa Barca, David Villa, aliyehama klabu hiyo majira haya ya joto, alitangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 12 kabla ya Neymar kutokea benchi na kusawazisha dakika ya 59 akiunganisha krosi ya Mbrazil. mwenzake, Dani Alves.

Majeruhi: Lionel Messi alitolewa nje baada ya kuumia katika mchezo wa Super Cup jana

Messi alikosa mechi kadhaa mwishoni mwa msimu uliopita kwa maumivu ya nyama mguu wa kulia

Bonge la kichwa: Neymar akiisawazishia Barcelona

Neymar akishangilia kuifungia klabu yake mpya, Barcelona aliyojiunga nayo kutoka kwa dau la Pauni Milioni 48


Amewaonyesha: David Villa akishangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani

David Villa aliifungia dakika ya 12 Atletico

Shangwe za Villa

Mshambuliaji wa Atletico, Diego Costa akipambana na Jordi Alba wa Barca

Kipa Thibaut Courtois na mabeki wake, Filipe na Diego Godin wakijaribu kumzuia Alexis Sanchez

Kiungo wa Atletico, Mario Suarez akimtoka mshambuliaji wa Barca, Sanchez

Mchezaji wa Atletico, Miranda akijiandaa kupiga mbele pembeni ya Pedro wa Barca


.png)