• HABARI MPYA

    Friday, August 30, 2013

    TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BILIONI 5.5 LIGI KUU BARA

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA AGOSTI 30, 2013 SAA 10:25 JIONI 
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Thys Torrington akimshuhudia Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani akisaini Mkataba huo. 

    Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
    Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
    Ulaji huu nimtengenezee Malinzi? Athumani Nyamlani kushoto atagombea Urais wa TFF dhidi ya Jamal Malinzi Oktoba, mwaka huu. Je, atakula matunda ya udhamini huu au atamuachia Malinzi?


    Wanabadilishana mikataba

    Mambo yameiva, sasa Ligi Kuu ndani ya Azam TV

    Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BILIONI 5.5 LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top