![]() |
| Twiga Stars |
KIINGILIO cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za
Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia
itakayochezwa Jumamosi (Juni 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni
sh. 2,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo, amesema kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu, kijani
na rangi ya chungwa. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji
48,590 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Amesema viingilio vingine kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10
kamili jioni ni sh. 5,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 10,000.
Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.
Amesema mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi Grace Msiska
atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Bernadettar Kwimbira, Happiness
Mbandambanda na Linda Chikuni, wote kutoka Malawi. Kamishna ambaye anatoka
Kenya ni Maqulate Atieno. Waamuzi hao wanawasili leo.
Wakati huo huo: Wambura amesema kwamba marefa 54
wanaoshiriki kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyoanza
Juni 11 mwaka huu, kesho (Juni 14 mwaka huu) watahamia Uwanja wa Karume kwa
ajili ya mazoezi ya alama (signals). Mazoezi hayo yatafanyika kuanzia saa 1-4
asubuhi.
Amesema kozi hiyo itakayomalizika kesho (Juni 14 mwaka huu)
inaendeshwa na wakufunzi Carlos Henriques na Mark Mizengo kutoka FIFA
wakisaidiwa na wakufunzi wengine wanne wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Amewataja Wakufunzi wa TFF ni Kapteni mstaafu Stanley
Lugenge, Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
Marefa wanaoshiriki ni 14 wa Tanzania wenye beji za FIFA
ambao ni Erasmo Jesse, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, Hamis Maswa, Israel
Mujuni, John Kanyenye, Josephat Bulali, Judith Gamba, Mwanahija Makame, Oden
Mbaga, Ramadhan Ibada, Saada Tibabimale, Samuel Mpenzu na Sheha Waziri.
Washiriki wengine ni 20 wa daraja la kwanza (class one),
kati ya hao watano wanatoka Zanzibar. Lakini vilevile wapo waamuzi chipukizi
(watoto) 20 ambao mwaka jana walitumika katika michuano ya Kombe la Uhai na
Copa Coca-Cola.



.png)
0 comments:
Post a Comment