• HABARI MPYA

    Thursday, June 28, 2012

    PREVIEW ITALIA NA UJERUMANI LEO

    Kocha wa Italia, Cesare Prandelli, ataendelea kucheka leo? 

    VIKOSI VYA LEO (Imetafsiriwa na Prince Akbar kutoka Goal.com)

    UJERUMANI

    Neuer
    Boateng, Hummels, Badstuber, Lahm
    Khedira, Schweinsteiger
    Reus, Ozil, Schurrle
    Klose
    ITALIA

    Buffon
    Abate, Barzagli, Bonucci, Balzaretti 
    Marchisio, Pirlo, Nocerino
    Motta
    Balotelli, Cassano

    KIUNGO wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger amepona maumivu ya kifundo cha mguu na usiku wa leo ataichezea nchi yake dhidi ya Italia.
    Nyota wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan, ambaye hajacheza mechi yoyote ya Euro 2012, aliuamia kifundo cha mguu katikia mazoedzi Jumamosi na yuko shakani kucheza.
    Kocha Joachim Low anaweza akashusha kikosi kile kile kilichomenyana na Ugiriki katika Robo Fainali.
    Mshambuliaji mkongwe, Miroslav Klose anatarajiwa kurejea katika nafasi yake mbele akicheza pamoja  na Mario Gomez, wakati kiungo Lars Bender anaweaza kuchukua nafasi ya Jerome Boateng katika beki ya kulia.
    Beki wa Italia, Giorgio Chiellini amerejea mazoezini baada ya kupona maumikvu ya nyama za paja na anaweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza, akichukua nafasi ya mchezaji mwenzake wa Juventus, Leonardo Bonucci.
    Kocha wa Azzurri, Cesare Prandelli pia anahofia uimara wa Daniele De Rossi na Ignazio Abate baada ya wawili hao kupata maumivu ya misuli katika mechi waliyoshinda kwa mikwaju ya penalti dhidi ya England, wakati Christian Maggio ana kadi.
    Kiungo wa Paris Saint-Germain, Thiago Motta amepona na anaweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza akichukua nafasi ya Riccardo Montolivo.
     JE WAJUA?

    • Ujerumani imeshinda mechi 15 mfululizo za mashindano, ikivunja rekodi ya mechi 14 iliyowekwa na Hispania (kati ya mwaka 2010 na 2011), Uholanzi (2008-2010) na Ufaransa (2002-2004).
    • Die Mannschaft hawajawahi kuifunga Italia katika mashindano. Rekodi yao katika mechi saba walizokutana kwenye michuano mikubwa ni sare nne na kufungwa tatu.
    • Mabingwa mara tatu, Ujerumani imeshinda mechi zake zote za Nusu Fainali, kasoro moja tu ya sita katika Kombe la Mataifa Ulaya.
    • Kikosi cha Joachim Low kimekuwa kikifunga angalau bao moha katika mechi kati ya mechi zao 20 zilizopita.
    • Italia imeshinda mechi moja tu kati ya saba zilizopita za hatua hii.
    • The Azzurri wanakutana na Ujerumani leo kwa mara ya  31, huku rekodi yao ya awali ni kushinda mechi 14, sare 9 na kufungwa 7. Hawajafungwa na wajerumani tangu wafungwe 2-0 katika mchezo wa kirafiki Juni mwaka 1995.
    • Italia hadi sasa haijapoteza mechi hata moja ya mashindano chini ya kocha Cesare Prandelli, aliyeiongoza timu hiyo kushinda mechi tisa na sare tano.
    • Andrea Pirlo (pichani kulia) aligawa pasi 146 katika Robo Fainali dhidi ya England, kati ya hizo 117 zilifika kwa walengwa- ambayo ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote katika Euro 2012 hadi sasa, zikiwemo za dakika za nyongeza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PREVIEW ITALIA NA UJERUMANI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top