Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya


MAN CITY BADO WATAKA KATIKA USAJILI

KLABU ya Manchester City inawawania wachezaji wa Newcastle, Fabricio Coloccini na wa Liverpool, Daniel Agger kama mbadala wa Joleon Lescott, ambaye anaweza kuondoka Eastlands.
Manchester City
Manchester City inamtaka Fabricio Coloccini kuchukua nafasi ya Joleon Lescott
KLABU ya Chelsea imemgeukia winga wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle, mwenye umri wa miaka 21, baada ya klabu ya Wigan kuvunja mazungumzo ya kumuuza Victor Moses.
KLABU ya Lazio ya Italia, ipo karibu kumsajili mchezaji anayewaniwa pia na West Ham na Tottenham, Burak Yilmaz, mwenye umri wa miaka 26, kwa mujibu wa taarifa kutoka Italia.
KIUNGO wa Chelsea, Raul Meireles, mwenye umri wa miaka 29, anatakiwa kwa dau la pauni Milioni 8 na klabu ya Serie A, Napoli.
KLABU ya Fiorentina imeghairi kumuuza mchezaji wao anayetakiwa na Liverpool na Aston Villa, Juan Manuel Vargas, mwenye umri wa miaka 28, baada ya klabu hizo kushindwa kufika bei inayotakiwa na klabu hiyo ya Italia,  pauni Milioni 12.
PENDEKEZO la Edin Dzeko kuhama Manchester City na kutua Bayern Munich liko shakani kutimia, kufuatia vigogo hao wa Ujerumani kutupa ndoana zao kwa mshambuliaji wa Wolfsburg, Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 26.
MKONGWE Craig Bellamy anaamini kocha Brendan Rodgers na Liverpool itakuwa  "uwili mtakatifu" - lakini Cardiff City inaweza kumng'oa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 katika viunga vya Anfield.

ENGLAND

MCHEZAJI wa zamani wa Southampton na England, Matt Le Tissier anaamini kutokuwa fiti kwa England ilikuwa sababu kubwa kwa Three Lions kutolewa kwenye Robo Fainali ya Euro 2012 na Italia.
TIMU ya taifa ya England, imepanga ziara fupi nchini Brazil msimu ujao sambamba na kucheza mechi za kirafiki na wenyeji hao wa fainali zijazo za Kombe la Dunia 2014 na majirani zao, Uruguay.
KOCHA Harry Redknapp amesema Engand itaendelea kuboronga kwenye michuano, hadi wachezaji wake watakapojifunza kutulia na mpira.

EURO 2012

KIUNGO wa Ujerumani, Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 23, amesema kwamba Hispania ina nafasi kubwa  ya kutwa ubingwa wa Euro 2012.

QPR KUMLIMA MISHAHARA MITATU BARTON

Scott Sinclair
Swansea City inatumaini Scott Sinclair atasaini mkataba mpya
KLABU ya QPR inataka kumpiga faini Joey Barton mshahara wa miezi mitatu  - pauni 840,000 - kwa kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya mwisho ya kufunga msimu uliopita dhidi ya Manchester City.
KLABU ya Swansea City ina matumaini Scott Sinclair, mwenye umri wa miaka 23, atasaini mkataba mpya kufuatia kuteuliwa kwa Michael Laudrup kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.

HART ALIANGALIA VIDEO GANI?

MASWALI yasiyo na majibu yameikbuka juu ya kipa wa England, Joe Hart ni video ipi haswa aliitazama kujiandaa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Italia.