• HABARI MPYA

    Thursday, June 28, 2012

    JEMBE LA THE CRANES LATUA SIMBS SC LEO


    Mussa Mudde anatua Msimbazi leo

    Na Prince Akbar
    KIUNGO wa kimataifa wa Uganda, Mussa Mudde aliyesajiliwa na mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC kutoka Sofapaka ya Kenya, anatarajiwa kuwasili leo kujiunga na wenzake kuendelea na maandalizi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, imeelezwa.
    Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’, ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba, mbali na Mudde kutarajiwa kutua leo, pia mshambuliaji wao waliyemsajili kutoka Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Mrwanda ataanza mazoezi rasmi leo.
    “Mazoezi yataendelea Sigara (TCC Chang’ombe) na pamoja na kumtarajia Mudde, lakini pia mshambuliaji wetu wa zamani, Danny Mrwanda aliyerejea kikosini, ataanza mazoezi kesho,”alisema jana usiku Kamwaga.
    Katika mazoezi ya Simba SC juzi na jana uwanja wa TCC, beki mpya wa klabu hiyo Masombo Lino, kutoka Daring Club Motema Pembe kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amekuwa kivutio kutokana na soka yake baab kubwa.
    Katika mazoezi yanayoendelea chini ya Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovick, Masombo amekuwa akionyesha ni mzuri kwenye kuzuia na kusaidia mashambulizi pia.
    Mazoezi ya Simba yanaendelea leo kwenye Uwanja huo, kujiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano iliyopangwa kuanza Julai 14 hadi 29, mwakani.
    Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lilitua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba. 
    Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wamemsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga.
    Wakati huo huo: Kamwaga amesema kuhusu kushiriki kwao au kutoshiriki michuano ya Kombe la Ujirani Mwema, inayoandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) wataamua leo.
    “Tutakuwa na kikao kesho, lazima tupitie ratiba ya mashindano hayo na tuangalie je haitatuathiri kwa ushiriki wetu kwenye Kombe la Kagame, maana Kagame nayo inafanyika mwezi huu pia,”alisema Kamwaga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JEMBE LA THE CRANES LATUA SIMBS SC LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top