Tetesi za J'pili magazseti ya Ulaya


MAN CITY KUTOA PAUNI MILIONI 52 KWA SILVA KUIKOMOA REAL

KLABU ya Manchester City iko tayari kujadili mkataba wa pauni Milioni 52 na kiungo wake mshambuliaji, David Silva - ili kupambana na Real Madrid wanaomtaka.
WINGA Gareth Bale, mwenyr umri wa miaka 22, ameamua kubaki katika klabu yake ya Tottenham yenye maskani yake White Hart Lane kwa angalau mwaka mmoja zaidi.
KLABU ya Manchester City inamtaka beki wa Kibrazi, Dede, mwenye umri wa miaka 23, katika mkakati wa kuiimarisha safu yao ya ulinzi baada yakocha Roberto Mancini kuamua kuachana na beki wa AC Milan, Thiago Silva.
MKONGWE Danny Murphy atajiunga na Blackburn Rovers baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 35 kumaliza mkataba wake na Fulham.
Luka Modric
Luka Modric anataka kutua Real Madrid
BEKI wa Sweden, Olof Mellberg anaweza kutua Everton. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34, aliyewahi kuchezea Aston Villa amemaliza mkataba wake na mabingwa wa Ugiriki,  Olympiakos.
MSHAMBULIAJI wa Newcastle, Leon Best, 25, amepata ofa ambayo itakuwa vigumu kwake kuikataa, kujiunga na Blackburn Rovers.
KLABU za Liverpool na Everton zimegongana sokoni, zote zikiisaka saini ya mshambuliaji wa Inter Milan, Luc Castaignos, mwenye umri wa miaka 19.
HATIMAYE Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, ameamua kuondoka Tottenham akacheze Hispania katika La Liga, tena klabu ya Real Madrid. Manchester United na Paris St-Germain nazo zilikuwa zinamtaka Modric, lakini inasemekana kiungo huyo wa Croatia moyo wake unapenda kufanya kazi na Jose Mourinho.

EURO 2012

KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello amechanganywa na habari kwamba amekuwa akiisaidia Italia maandalizi ya mechi ya Robo Fainali ya Euro 2012 leo dhidi ya England.
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya England hawawezi kuogopa kumkaba Mario Balotelli - kwa sababu mchezaji huyo ni kimeo na anaweza kulimwa yeye mwenyewe kadi nyekundu wakati wowote, kwa mujibu wa kocha  Gary Neville.
Andre Villas-Boas
Andre Villas-Boas
Mario Balotelli amewaambia wachezaji wenzake wa Manchester City  na wapinzani wao England kwamba hamuogopi yeyote kati yao kuelekea mechi ya leo ya Robo Fainali ya Euro 2012 mjini Kiev.

AVB NA BLANC SPURS...

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas anapambana na makocha watatu kuwania kazi Spurs, wakiwemo kocha wa zamani wa Schalke, Ralf Rangnick na Laurent Blanc, anayeinoa Ufaransa kwa sasa ambayo jana imetolewa Euro 2012.