• HABARI MPYA

    Monday, June 25, 2012

    NGUZA ALIA TOKA GEREZANI; SIJAPATA HATA SENTI YA WIMBO SEYA


    Nguza kulia akiwa na mwanawe, Papii

    MWANAMUZIKI nguli wa dansi nchini, Nguza Viking amesema kutoka gereza la Ukonga kwamba, hajagusa hata senti moja kutokana na mauzo ya wimbo wake Seya na hajui fedha zilienda wapi.
    Nguza ambaye gerezani anatumikia kifungo pamoja na wanawe akikwemo Papii Kocha aliyerekodi naye wimbo huo kwa mara ya pili, jana alitembelewa gerezani na mwanamuziki mwenzake, John Kitime.
    Kitime aliporejea kutoka Gerezani, akaandika kwenye blog yake; “Nimekwenda gereza la Ukonga asubuhi hii (jana) kumsalimia Nguza na mwanae Papii, nimewakuta wachangamfu wenye afya nzuri. Nguza kanituma NIWASALIMIE WOTE, naomba nitumie jukwaa hili kutangaza salamu hizo,”.
    Nguza enzi za ujana wake
    “Ni wazi italazimika kuomba muda wa ziada kutoka kwa uongozi wa Magereza kuzungumza zaidi na Nguza, jambo mojawapo ambalo tutalizungumza ni kuhusu mapato ya wimbo wa Seya. Pamoja na umaarufu wote ni jambo la kusikitisha kuwa Nguza anasema hajapata fedha yoyote kutoka wimbo ule, zaidi ya fedha alizopewa kuingia studio kuurekodi. Swali ni nani anazipokea fedha za wimbo ule?”ameandika Kitime.
    Hii itakuwa kashfa nyingine kubwa kwa wadau wakubwa wa muziki Tanzania, kwani wimbo huo ulikuwa katika mradi ulioandaliwa na jamaa mmoja maarufu sana katika medani ya sanaa na burudani, anayeaminika hadi Ikulu, uliotwa Baba na Mwana.
    BIN ZUBEIRY haitaki kujikita sana kwenye suala hilo, ila inakaribisha mjadala tena mpana tu, labda njia itapatikana.
    Nguza wanawe, walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa kumi ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya Aprili na Oktoba mwaka 2003 maeneo ya Sinza mjini Dar es Salaam.
    Mwishoni mwa mwaka 2009, Babu Seya na wanawe Papii Nguza 'Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walikata rufaa dhidi ya hukumu ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Addy Lyamuya, lakini akaachiwa mtoto wake mmoja tu, Francis ‘Chichi’. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGUZA ALIA TOKA GEREZANI; SIJAPATA HATA SENTI YA WIMBO SEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top