• HABARI MPYA

    Monday, June 25, 2012

    ALONSO ATAKATA LANGALANGA


    24 Juni, 2012 - Saa 15:31 GMT
    Fernando Alonso
    Fernando Alonso

    ferrari
    Ferrari la Alonso


    DEREVA wa magari ya Timu ya Ferrari Fernando Alonso amekua dereva wa kwanza kushinda mara mbili mwaka huu kwa ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya Ulaya.
    Yeye Alonzo alianza katika nafasi ya 11 kabla ya gari la usalama kuingilia mashindano kufuatia ajali lakini juhudi zake zilimuezesha kupambana hadi nafasi ya nne.
    Aliweza kuongoza kufuatia mizengwe iliyotokea ndani ya kituo cha magari ya McLaren ambako wakati wa kubadili tairi na kuongezea mafuta Hamilton alipoteza zaidi ya sekundi 14 na kwa bahati nzuri dereva aliyekua akiongoza Sebastien Vettel akashindwa kumaliza mbio hizo.
    Kimi Raikkonen alimaliza wa pili, il hali Hamilton akikwama ikisalia mizunguko miwili baada ya kukwaruzana na Pastor Maldonaldo wa timu ya magari ya Williams.
    Hadi hapo Hamilton alikua akishikiliaa nafasi ya pili akijitahidi kumaliza katika nafasi hio licha ya tairi kuishilia kwa kasi na Maldonaldo alimuingilia na kulichana gari kiasi kwamba halingeweza kuendelea na mbio.
    Ushindi wa Alonzo ni wa 29 ukimweka tangu aane kushiriki mbio za magari na unamuweka kileleni mwa Madereva bora akiwa na pointi 20, Mark Webber ni wa pili na Hamilton wa tatu, Vettel anashikilia nafasi ya nne akiwa nyuma ya Alonzo kwa tofauti ya pointi 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALONSO ATAKATA LANGALANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top