Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya


MANCHESTER CITY YAWATAKA EDINSON CAVANI NA FALCAO

KLABU ya Manchester City inatafakari juu ya kuwasajili nyota wa  Napoli, Edinson Cavani, mwenye umri wa miaka 25 na nyota wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, mwenye umri wa miaka 26.
KLABUI za Everton na West Brom zinaagalia uwezekano wa kumalizana na Rangers juu ya wachezaji Steven Naismith, mwenye umri wa miaka 25, na Steven Whittaker, mwenye umri wa miaka 28. Wanasoka hao wa kimataifa wa Scotland wote wamekataa kuhamishwa kutokana na mikataba yao na klabu hiyo ya SPL.
KLABU ya Blackburn inataka kubeba wachezaji wawili kutoka Newcastle, Dan Gosling, mwenye umri wa miaka 22 na Leon Best, mwenye miaka 25, katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kocha Steve Kean.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema yuko kwenye mkakati wa kumtwaa mshambuliaji wa Ujerumani, Marco Reus. Bosi huyo wa Arsenal, amesema hayo kuhusu Reus, mwenye umri wa miaka 23, wakati akiizungumzia mechi ya Euro 2012 kati ya Ujerumani na Ugiriki kwenye TV ya Ufaransa.
KLABU ya Barcelona inataka kumchukua kinda wa Manchester City, Joan Angel Roman.  Angel Roman, mwenye umri wa miaka 19, alikwenda City miaka mitatu iliyopita akitokea Espanyol, lakini hajatimiza malengo yake.
KLABU ya Cardiff inafanya mipango ya kumrejesha Craig Bellamy. Tajiri wa klabu hiyo kutoka Malaysia anamtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, awasaidie harakati za kupanda msimu ujao.
KLABU za West Brom na Newcastle zote zanamnyemelea kwa mkopo  beki wa pembeni wa Tottenham, Danny Rose, mwenye umri wa miaka 21. Spurs inatarajiwa pia kumpoteza beki mwingine wa pembeni, Vedran Corluka.

EURO 2012

KOCHA wa England, Roy Hodgson amesema hakukuwa na cha ziada cha kufanya wakati Three Lions wakitolewa kwa mara ya tano mfululizo kwa mikwaju ya penalti.
MAANDALIZI ya Ujerumani kuelekea mechi ya Nusu Fainali Alhamisi yameingia doa baada ya kubainika vikosi vya timu hiyo vimekuwa vikivuja kwenye vyombo vya habari kabla ya mechi.
MUSTAKABALI wa Samir Nasri katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kutokana na Chama cha Soka cha Ufaransa kukerwa na ishara aliyowafanyia Waandishi wa Habari.

CLARK B'NGHAM

KLABU ya Birmingham ina matumaini ya kumtambulisha Lee Clark kama kocha wao mpya. Brum wanamtaka Clark, mwenye umri wa miaka 39, awe kocha wao mpya baada ya kumpoteza Chris Hughton aliyehamia Norwich.