• HABARI MPYA

    Wednesday, June 13, 2012

    AZAM IKO TAYARI KUWAPA YANGA SURE BOY JR.


    Sure Boy Je kazini Azam

    UONGOZI wa klabu ya Azam FC umeipa ruhusa Yanga kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo, Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’, lakini tu waende na ofa ya kueleweka.
    Meneja wa Azam FC, Patrick Kahamele ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, sera ya Azam si kuwazuia wachezaji wanaotaka kuondoka, lakini wanataka taratibu zifuatwe.
    “Yanga kama wanamtaka Sure Boy walete barua rasmi ya maombi, tena waje na ofa ya maana, tutawauzia,”alisema Kahamele.
    Sure Boy Jr. aliyeng’ara kwenye mechi ya Taifa Stars na Gambia Jumapili, Uwanja wa Taifa, akicheza kwa uelewano mkubwa na Frank Damayo na Mwinyi Kazimoto katika safu ya kiungo, ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’.  
    Mwaka jana, Yanga waliomba kumsajili Mrisho Ngassa kutoka Azam, lakini wakakwama kutoka dau lao dogo, Sh. Milioni 25. Azam pia imesema hata Ngassa wako tayari kumuacha aende Yanga, iwapo watatoa ofa nzuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM IKO TAYARI KUWAPA YANGA SURE BOY JR. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top