• HABARI MPYA

    Tuesday, March 03, 2020

    NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

    Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM 
    UONGOZI wa Klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji wake wa zamani, Damian Mrisho Kimti aliyefariki dunia jana jioni Jijini Dar es Salaam.
    Kimti alikuwa mmoja wa wachezaji ambao walicheza mchezo wa fainali ya ubingwa wa Afrika Mashariki mwaka 1992 ambao tuliibuka na ushindi dhidi ya Yanga na pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 dhidi ya Stella Abidjan.
    Klabu itamkumbuka Kimti kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwetu kwa kipindi chote ambacho alikuwa akichezea timu yetu.
    Damian Kimti (kulia) akivalishwa Medali na aliyekuwa Waziri wa Michezo, Profesa Philemon Sarungi baada ya fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 

    Klabu ya Simba inaungana na familia pamoja na wadau wa mpira wa miguu katika msiba huu. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na msiba huu.
    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top