• HABARI MPYA

  Monday, July 01, 2019

  SERGE WAWA PASCAL ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUENDELEA NA KAZI SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI Muivory Coast, Serge Wawa Pascal amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea klabu ya SImba ya Dar es Salaam.
  Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba, Wawa amepewa mkataba mpya baada ya kazi yake nzuri msimu uliopita iliyompendezea kocha Mbelgiji, Patrick Aussems.
  “Pascal Wawa ni rasmi sasa kwamba ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa wa nchi baada ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja,”imesema taarifa ya Simba SC.
  Wawa anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliosaini mikataba mipya, wakiwemo kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala, viungo Jonas Mkude, Mzambia Clatous Chama na washambuliaji Nahodha Mkuu, John Bocco na Meddie Kagere raia wa Rwanda.

  Pamoja na kuwaongezea mikataba wachezaji wake msimu uliopita, Simba SC pia imesajili wachezaji wapya saba wakiwemo Wabrazil watatu, mabeki beki Gerson Fraga Vieira ATK ya Ligi Kuu ya India na Tairone Santos da Silva kutoka klabu ya Atletico Cearense FC, mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva kutoka Bragantino, zote za Daraja la Nne nchini Brazil.
  Wengine ni kipa Beno Kakolanya kutoka Yanga, beki Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United za nyumbani, kiungo Msudan na Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERGE WAWA PASCAL ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUENDELEA NA KAZI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top