• HABARI MPYA

  Monday, July 01, 2019

  YANGA SC YAUNDA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO, YAITA CHIPUKIZI USAILI WA U17 NA U20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa klabu Yanga SC ya Dar es Salaam, Dk. Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya klabu wameunda Kamati ya Fedha na Mipango.
  Taarifa ya klabu kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba Kamati hiyo itakuwa chini ya Mwenyekiti, Arafat Hajji, Makamu wake, Shijja Richard na Katibu Deo Mutta.
  Wajumbe wa Kamati hiyo ni Said Kambi, Ally Mayay, Pindu Luhoyo, Baraka Katemba, Suma Mwaitenda, Haruna Batenga na Ivan Tarimo.
  Wakati huo huo: Uongozi wa Yanga SC umeitisha wachezaji chipukizi wenye vipaji vya soka kujitokeza kwenye usaili wa kuunda timu za vijana za klabu hiyo chini ya miaka 17 na U20.

  Nahodha wa zamani wa Yanga, Ally Mayay ameteuliwa Kamati ya Fedha na Mipango

  Taarifa ya Yanga imesema kwamba zoezi hilo litafanyika kuanzia Julai 4 hadi Julai 7, mwaka huu viwanja vya Fire, Upanga mjini Dar es Salaam na litawahusu vijana waliozaliwa kuanzia mwaka 2002.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAUNDA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO, YAITA CHIPUKIZI USAILI WA U17 NA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top