• HABARI MPYA

    Friday, July 05, 2019

    MSIMU MPYA WA LIGU KUU WAJA, SIMBA NA YANGA ZIPO TAYARI?

    Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
    HII ni julai au kwa kiswahili ni mwezi wa saba ni kama kipindi cha pili kuelekea kwenye mwisho wa mwaka,lakini kwa upande wa pili ni mwezi wa maandalizi kuelekea kwenye msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara na michuano ile ya kimataifa kwa maana ya michuano ya mabingwa na kombe kombe la shirikisho barani Afrika.
    Ni mwezi ambao hisia na shauku za mashabiki wa soka hapa Tanzinia uwa juu sana kwani kila timu inaamini na kuaminishwa kua wamesajili vifaa vya nguvu na msimu uanze ili wazishikishe adabu timu pinzani na ile mechi ya wao na sisi lini utamaniwa zaidi kwani ndio kipimo cha usajili na maandalizi bora kwa mashabiki wa Simba sc na Yanga sc kwani hawa ndio wenye mpira wa Tanzania na sidhani kama unaweza kuwakwepa uku ukiwa Tanzania labda uhamie malawi.

    Ndani ya wiki ya pili ya mwezi huu timu hizi kubwa zitaanza kambi kujiandaa na msimu ujao uku zikiwa na sura ngeni nyingi kwa ajili ya kuleta kitu kipya lakini si hivyo tu bali maandalizi ya kambi zao huwa murua sana si ajabu kusikia zikipaa na kwenda barani ulaya,asia na maeneo mengine kwa ajili  ya maandalizi lakini upande wa pili kuna yale matamasha makubwa kwa maana ya Simba day  ambalo uwa mwezi wa 8 tarehe 8 na lile la wiki ya mwananchi ambalo litafanyika mwezi huu wa  7 tarehe 27, pia kutakua na mechi za kirafiki na timu mbalimbali ili kuona uimara wa vikosi vyao..
    Kwanini nimegusia hayo yote ni kwa sababu zifuatazo..Ukiangalia timu zote mbili hizi kubwa zimesajili zaidi ya wachezaji 8 ambao kwa namna moja au nyingine wanakuja kuimarisha vikosi vyao na sidhani kama wamesajiliwa waje kukaa benchi hivyo mabenchi ya ufundi yanahitaji muda wa kutosha ili kuziandaa timu kwani kwa kiwango cha wastani inatakiwa kupatikana kuanzia wiki 6 ili timu iwe na maandilizi ya kutosha uku ikipata utulivu wa hali ya juu kuwawezesha waalimu na wataalamu wengine kutimiza majukumu yao mana kazi ni kubwa kuanzia kurudisha na kutengeneza utimamu wa miili ya wachezaji ukizingatia wametoka mapumzikoni lakini pia kuanza kutengeneza muunganiko wa hawa wachezaji katika maeneo yote ukizingatia kuna maingizo mapya mengi zaid ya nane hivyo unahatajika mda wa kutosha kwa kuikamilisha hiyo kazi na  kubwa ni kugundua vitu vya ziada walivyo navyo wachezaji uku kujaribu kuweka uwiano ulio sawa wa kasi na mienendo ndani na nje ya uwanja ili neno timu liwe na maana zaidi..
    Sasa kama hayo hayatazingatiwa maana yake maandalizi hayatakua yamekidhi vigezo na kupelekea timu kuanza msimu zikiwa hazipo sawa na pengine kupelekea matokeo yasiyo tarajiwa kutoka kwa wapenzi wa soka wa timu hizi na hapo ndipo ile migogoro isiyo kwisha inapoanzia.
    Upande mwingie nirudi kwa mashabiki wa timu hizi ni lazima mtambue kua ligi ni moja na bingwa ni mmoja pia,na mchezo wa mpira una matokea matatu kushinda sare na kupoteza na matokeo haya ni khaki kwa kila timu hivyo kuingia na matokeo yenu uwanjani si sawa na si khaki mwisho wa siku timu zikipoteza mnatafuta sababu za nje ya mpira na kuleta vurugu jambo linalowafanya viongozi wakati wote kuangaika kutuliza hasira zenu na kutafuta hata njia za mikato ili tu kuwapatia furaha na kuachana na mipango ya mda mrefu kwa maendeleo endelevu ya timu husika..
    Kingine ni lazima mtambue kua mchezaji mzuri sehemu moja anaweza asiwe mzuri sehemu nyingine kutokana na sababu nyingi sana,ugeni,mazingira,mifumo na mambo mengine mengi na kuhitaji mda wa kuthibitisha kile kilichowafanya mumsajili hivyo swala la mda linahusika sana kwa kuwavumilia na kuwatia moyo badala ya kuwapa presha kubwa ili tu watimize furaha zetu na badala ya kuwajenga mnawatoa mchezoni na kuonekana si kitu jambo linalopekea kila msimu timu zenu zinatoa watu na kuingiza watu hivyo unakuwa mwendo wa kujenga timu kila msimu..
    Pia timu hizi bado hazina vyanzo vya kudumu vya mapato ili kuweza kukidhi mahitaji ya msingi ya endeshaji hivyo ngozo kubwa ni viingilio vinavyopatikana baada ya ninyi kuingia uwanjani nimeona orodha ya mapato ya viingilio vya msimu uliopita nimesikitika sana kwa uwingi wa mashabiki mlivyo na kelele zinazopigwa hakuna timu ambayo imekusanya zaidi ya milioni walau 800 kwa jumla katika mechi zote 38.ni jambo la kushangaza sana kwani bila ubisha kila mkoa hizi timu zinamashabiki wa kutosha ambao kama kweli wakiamua kujitoa kufatilia mechi za timu zao kwa kwenda uwanjani nina uhakika timu zitakusanya zaidi ya bilioni moja.
    Kuna jamaa ananiambia hapa kuwa timu mwenyeji ndiyo huchukua mapato ya mchezo wa nyumbani hivyo badala ya mechi 38 niseme 19 tu hapana mimi nasema 38 kwani ukiacha viingilio bado kuna biashara ya jezi,scafu,kofia na vitu kibao ambavyo vinauzwa  viwanjani nje ya viingilio ambavyo vinaweza ongeza pato lakini pia mechi nyingi za hizi timu zimechezwa uwanja wa taifa ambao unachukua zaidi ya watu elfu 60 hivyo walau wakifika watu elfu 50 kwa mechi 19 bado hesabu ya bilioni inafikiwa na ndio njia ya kweli ya kuzifanya timu ziende,ila kushabikia uku ukiwa hauna mchango wowote kwenye timu zaidi ya kulaumu viongozi na kufikia kutoa lugha chafu haisaidii na haijengi toa mchango wako kwa kulipia tiketi na kununua bidhaa za timu yako halafu ndio uwe mkali timu ikivurunda ukiwa wewe unatoa.
    Ebwana kesho nayo si siku ngoja tuachie hapa ila kila timu imejinasibu kuwa ipo tayari kilichobaki ni SISI NA WAO LINI NDANI YA TAIFA?
    (Unaweza kumfollow mwandish wa makala hii kwa @dominicksalamba au kumpigia simu namba +255713942770)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSIMU MPYA WA LIGU KUU WAJA, SIMBA NA YANGA ZIPO TAYARI? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top