• HABARI MPYA

  Monday, July 01, 2019

  MO-XTRA YAMWAGA SH. MILIONI 250 KUIDHANINI SIMBA, TIMU KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI

  Na Saada Akida, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa klabu ya Simba umeingia mkataba wa mwaka moja wenye thamani ya Milioni 250 kupitia kinywaji cha Mo Xtra ambayo watakuwa wadhamini wao badala ya Mo Energy.
  Simba msimu uliopita waliingia mkataba na A One iliyopo chini ya Kampuni ya Mohammed Intepres kupitia kinywaji chake kipya cha Mo Xtra. 
  Akizungunza na Waandishi wa habari jijini Jana, Mkurugezi wa Masoko wa METL, Fatma Dewji alisema udhamini huo ni muendelezo waliingia mwaka jana kupitia kinywaji cha Mo Energy.
  Alisema Mwaka huu wanaendelea na udhamini huo kupitia kinywaji Xtra waki imani itawasaidia na uendekeza walipoishia Mwaka Jana.
  "Udhamini wa Mwaka Jana tumeona faida yake simba ilifika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na kutetea taji lao la ubingwa," alisema.
  Fatma alisema wana imani udhamini wa Mwaka huu watafikia malengo Yao ikiwemo kutetea ubingwa bara pamoja na kucheza fainali za Afrika.
  Wakati huo huo: Kikosi cha Simba kinatarajiwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi yao ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Simba awali walipanga timu yao hiyo kwenda nchini Marekani na baade walibadilisha mawazo hayo huku wakiteuwa nchini Nne ikiwemo Afrika kusini, Misri, Ghana na Zimbabwe.
  Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Bodi hiyo kwamba wamejadiliana na wametoa maamuzi ya kwenda Afrika Kusini ambayo ni karibuni na rahisi kupata timu za kucheza mechi za kirafiki.
  Alisema Afrika Kusini watakuwa karibu na  wameanza utaratibu wa kufanya mchakato wa kuangalia sehemu tulivu ikiwemo Hotel na mahala ya uwanja wa kufanyia mazoezi ikiwa ni maandalizi ya msimu  mpya.
  "Unajua suala la kambi ilikuwa bado tukijadiliana sana ni wapi timu iende, hivyo katika nchi zile na kuona bora waenda Afrika Kusini maana ni karibu na tutapata timu za kucheza nazo mechi za kirafiki za ushindani," alisema Kigogo huyo.
  Alipoulizwa Afisa Mtendaji Kuu wa Simba, Crescentius Magori kuhusu kambi alisema bado wako katika majadiliano na Bodi na baada ya kukubaliana ataweka wazi ni nchi gani ambayo timu itaenda kufanya maandalizi.
  "Kwa sasa tupo katika usajili lakini pia tunajadiliana ni wapi msimu huu timu ikaweke kambi , suala la nchi itajulika kama baada ya kukamilisha vikao gay Bodi ya Simba," alisema Magori.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MO-XTRA YAMWAGA SH. MILIONI 250 KUIDHANINI SIMBA, TIMU KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top