• HABARI MPYA

  Tuesday, October 02, 2018

  ZAHERA ANATAKA MAKAMBO AFUNGE MABAO 15 MSIMU MZIMA YANGA, KWA AJIB NA KASEKE NANE YATATOSHA

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amemtaka mshambuliaji wa timu hiyo, Heritier Makambo kufunga mabao yasiyopungua 15 katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Zahera ambaye kama Makambo wote wanatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amesema anaamini hicho ni kipimo tosha kwa mshambuliaji bora. 
  Lakini Zahera ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya DRC, amesema kwamba kwa viungo wake washambuliaji Ibrahim Ajibu na Deus Kaseke anahitaji kila mmoja afunge angalau mabao manane, wakati viungo wengine wa katikati Mkongo mwenzake, Papy Kabamba Tshishimbi na Feisal Salum 'Fei Toto' anataka kila mmoja afunge mabao yasiyopungua matano hadi mwishoni mwa msimu.

  Heritier Makambo (kulia) anatakiwa kufunga mabao yasiyopungua 15 msimu huu wa Yanga SC

  “Nataka huyu Makambo mshambuliaji wa kati afunge magoli kuanzia 15, hawa wanaotokea pembeni Ajibu na Kaseke wafunge magoli kuanzia nane na viungo wa kati, Tshishimbi na Feisal Salum nataka magoli yasiyopungua matano kila mmoja,”alisema kocha huyo aliyejiunga na Yanga SC Julai mwaka huu.
  Wakati Yanga SC imekwishacheza mechi tano tu za Ligi Kuu, ikishinda nne na sare moja, Makambo ndiyo kwanza ana mabao mawili tu, sawa na mshambuliaji mwingine, Mrundi, Amissi Tambwe, wakati Ajibu na Kaseke kila mmoja ana bao moja sawa na mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa – na Tshishimbi na Feisal bado hawajafumania nyavu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAHERA ANATAKA MAKAMBO AFUNGE MABAO 15 MSIMU MZIMA YANGA, KWA AJIB NA KASEKE NANE YATATOSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top