• HABARI MPYA

  Monday, October 01, 2018

  MTIBWA SUGAR YAPANDA TENA KILELENI LIGI KUU, YANGA SC SASA YA TATU NYUMBA YA MBAO FC

  TIMU ya Mtibwa Sugar imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo uliofanyika mchana wa leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro mchana wa leo.
  Ushindi huo unaifanya Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila ifikishe pointi 16 baada ya kucheza mechi nane, ikifuatiwa na Mbao FC yenye pointi 14 za mechi saba na Yanga SC pointi 13 za mechi tano.
  Mabao ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo yamefungwa na Salum Kihimbwa dakika ya 41 na Haroun Athumani Chanongo dakika ya 82, wakati la Biashara United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu limefungwa na Daniel Manyeye dakika ya 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAPANDA TENA KILELENI LIGI KUU, YANGA SC SASA YA TATU NYUMBA YA MBAO FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top