• HABARI MPYA

  Monday, October 01, 2018

  MECHI YA WATANI JADI YAINGIZA SH MILIONI 404, SIMBA SC WAPEWA MILIONI 200 YANGA HADI MWAKANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO namba 72 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga SC uliochezwa Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam umeingiza jumla ya Shilingi 404,549,000.
  Kiasi hicho kimetokana na watazamaji 50,168 waliokata tiketi na kati ya fedha hizo, wenyeji Simba SC wamepata karibu Sh. Milioni 200, wakati Yanga SC watachukua mapato ya mechi ya marudiano.
  Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni umeingiza jumla ya Watazamaji 50,168.
  Hekaheka katika mchezo wa jana ni wachezaji wa Simba SC dhidi ya wachezaji wa Yanga

  Mgawanyo wa mapato hayo ni kwenye upande wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), wauza tiketi, Selcom, TFF wenyewe, Uwanja, Simba, TPLB, gharama za mchezo, BMT na DRFA.
  Kati ya fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi 61,710,864.41, Selcom 17,901,293.25, TFF 16, 246,842.12 na Uwanja 48,740,526.35.
  Wenyeji wa mchezo Simba SC 194,962,105.41, TPLB 29, 244,315.81, gharama ya mchezo 22,745,578.96, BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA WATANI JADI YAINGIZA SH MILIONI 404, SIMBA SC WAPEWA MILIONI 200 YANGA HADI MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top