• HABARI MPYA

  Monday, February 01, 2016

  'WAJEDA' RUVU SHOOTING WAREJEA LIGI KUU KWA KISHINDO...RANGERS NAYO YANUKIA

  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameipongeza Ruvu Shooting ya Pwanji kwa kufanikiwa kupanda tena Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
  Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Kanali Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
  Ruvu Shooting imekuwa timu ya kwanza kujihakikishia tiketi ya Ligi Kuu msimu ujao, baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha pointi 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika hilo la B.

  Ligi Daraja la Kwanza imechezwa katika makundi mawili, na baada ya Kundi B kutoa timu ya kupanda sasa kimbembe kimebaki katika Kundi A, ambako timu za African Lyon, Ashanti United na KMC FC na Firends Rangers zinachuana kuwania nafasi hiyo.
  Kila timu ikiwa imebakiza mechi mbili, African Lyon inaongoza kwa pointi zake 23, ikifuatiwa na Ashanti United 22, KMC 21 na Rangers 20, wakati Kiluvya United yenye pointi 19 nayo ina nafasi pia ya kupanda kutoka kundi hilo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'WAJEDA' RUVU SHOOTING WAREJEA LIGI KUU KWA KISHINDO...RANGERS NAYO YANUKIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top