• HABARI MPYA

    Thursday, July 03, 2014

    SUAREZ NJIA MOJA CAMP NOU, MAZUNGUMZO LIVERPOOL NA BARCELONA YAFIKIA PAZURI, ALEXIS SANCHEZ KUTUA ANFIELD

    KLABU za Liverpool na Barcelona zitakuwa na mazungumzo mazito juu ya kuuziana Luis Suarez wiki hii baada ya klabu ya Hispania kutoa ofa ya wazi ya Pauni Milioni 72.
    Bado dau hilo ni dogo kulingana na like wanalotaka Liverpool, Pauni Milioni 80, lakini linaonyesha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko njiania kuondoka.
    Kikao cha jana mjini London kilikuwa kilichozalisha rasmi mpango wa biashara hiyo kwa panda zote mbili.
    Atakavyoonekana: Hivi ndivyo ambayo Suarez ataonekana akiwa amevalia jezi ya Barcelona, iwapo mpango wa uhamisho wake utakamilika

    Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre alikutana na mawakala wa nguvu wa Barcelona, Raul Sanllehi, Toni Rossich na Jordi Mestre.
    Pamoja na hao hakuna kilichokamilishwa ila kuna matarajio maafikiano yatafikiwa na Suarez anaweza kuhamia Barcelona.
    Liverpool imeendeleza nia yake ya kumtaka Alexis Sanchez na anaweza akajumuishwa katika mango huo huku Liverpool tayari ikiwa imemthaminisha kwa Pauni Milioni 30.
    Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile bado hajapewa taarifa coyote kuhusu kuhamia Anfield na uhamisho wa Suarez hauwezi kukamilishwa hadi nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aamue kujiunga na Liverpool, au Arsenal, ama klabu nyingine Ulaya au kubaki Nou Camp.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ NJIA MOJA CAMP NOU, MAZUNGUMZO LIVERPOOL NA BARCELONA YAFIKIA PAZURI, ALEXIS SANCHEZ KUTUA ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top