• HABARI MPYA

    Monday, July 07, 2014

    REAL MADRID WAPATA MSIBA MZITO, MCHEZAJI WAO NYOTA WA ZAMANI AFARIKI DUNIA LEO

    ULIMWENGU wa soka umepata pogo  kufuatia kifo cha gwiji wa Real Madrid, mshambuliaji Alfredo Di Stefano aliyefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 88. 
    Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Argentina na Colombia aliopatwa na ugonjwa wa moyo karibu na Uwanja wa klabu hiyo, Bernabeu Jumamosi mchana na akafariki dunia mchana wa leo. 
    Bingwa wa Ulaya: Alfredo di Stefano wa Real Madrid akiwa na makombe matano ya Ulaya, amefariki dunia leo
    Sad loss: Real Madrid's Alfredo Di Stefano celebrates with the original European Cup after Real beat Reims 4-3 in the 1956 final in Paris
    Pigo kubwa: Gwiji wa Real Madrid, Alfredo Di Stefano akisherehekea na Kombe halisi la Ulaya baada ya Real kuifunga Reims 4-3 katika fainali mwaka 1956 mjini Paris

    WASIFU WA DI STEFANO

    1945–1951 River Plate Mechi 66 Mabao 49
    1951–1953 Millonarios Mechi 102 Mabao 90
    1953–1964 Real Madrid Mechi 282 Mabao 216
    1964–1966 Espanyol 
    Mechi 47 Mabao 11
    Rais huyo wa heshima wa Real Madrid aliwekwa chumba cha wagonjwa maalum, akipatiwa tiba makini, lakini haikusaidia kuirejesha hali yake vizuri. 
    Amekuwa katika hali mbaya mno tangu Jumamosi alipofikishwa hospitali ya General Universitario Gregorio Maranon mjini Madrid. 
    Jitihada za madaktari bingwa wa hospitali hiyo kuokoa maisha ya gwiji hiyo hazikufanikiwa na hatimaye mchana wa leo akaaga dunia. Kikosi cha magwiji wa Real Madrid kinatarajiwa kuwa na ziara nchini mwezi ujao kwa mwaliko wa makampuni ya TSN, chini ya Mkurugenzi wake, Farough Baghozah.
    Legendary status: Di Stefano, here raising his glass during a tribute for his contribution to sport at the Argentina Embassy in Madrid, is Real Madrid's second highest goalscorer of all time
    Pumzika kwa amani gwiji: Di Stefano hapa akiinua bilauri yake wakati wa hafla maalum ya kumuenzi kwa mchango wake katika soka, iliyofanyika Ubalozi wa Argentina mjini Madrid. Ndiye mfungaji bora wa pili kihistoria Real Madrid.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL MADRID WAPATA MSIBA MZITO, MCHEZAJI WAO NYOTA WA ZAMANI AFARIKI DUNIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top